TANGAZO


Monday, December 1, 2014

TMF yafadhili waandishi wa habari tisa kwenda Accra nchini Ghana kupata mafunzo ya Habari za Biashara


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura, akizungumza wakati wa kuwaaga waandishi wa habari wanaosafiri kwenda Accra, Ghana kwa mafunzo ya Habari za Biashara.
Mkufunzi wa Masuala ya Habari za Biashara kutoka Accra Ghana, Nuamah Eshun (katikati), akizungumza katika hafla ya kuwaaga waandishi wa habari hao, Dar es Salaam leo asubuhi, kabla ya kuondoka kwenda nchini humo kwa mafunzo hayo ya siku 10. Eshun atakuwa ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Misaada wa TMF, Alex Kanyambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
Baadhi ya waandishi wa habari waliopo katika safari hiyo ya mafunzo.


Waandishi wa habari, wanaosafiri wakimsikiliza Mkufunzi wa Masuala ya Habari za Biashara kutoka Ghana, Nuamah Eshun.
Waandishi wa habari hao, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa safari hiyo leo.
Waandishi wa habari hao, wakienda kupanda gari leo, tayari kwa safari ya kwenda Accra nchini Ghana kwa mafunzo ya siku 10 kwa ufadhili wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF).
Na Dotto Mwaibale
MFUKO wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), umewafadhili waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwenda Accra nchini Ghana kupata mafunzo. 
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo katika maeneo ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi vyao kama namna ya kuchochea mabadiliko ya kimfumo katika vyombo vyao.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanahabari hao wapatao 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TMF Upanga Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura alisema TMF imekuwa ikiwawezesha wanahabari kupata mafunzo ya aina mbalimbali ndani nan je ya nchi.

Alisema wanahabari hao wanakwenda nchini humo ambapo watapata mafunzo kwa siku 10 kuanzia Disemba 2 hadi 13 mwaka huu.

"Waliochaguliwa kwenda kupata mafunzo hayo ni baadhi ya wakuu wa vitengo kutoka vyombo vya habari, mameneja, wamiliki wa vyombo vya habari na maofisa masoko na mauzo na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio" alisema Sungura.

Aliongeza kuwa tangu mwaka 2008 TMF imeweza kufadhili vyombo zaidi ya 120 na wanahabari zaidi ya 500 kupitia aina ya ruzuku mbalimbali. Kati ya vyombo 120 vilivyofadhiliwa na TMF, 31 vimepewa ruzuku inayolenga kuimarisha utendaji wao katika masuala ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi mbalimbali.

Alisema katika safari hiyo vituo vya redio vitano vimebahatika kuchaguliwa ambavyo ni CG Fm (Tabora), Standard FM (Singida), Kahama FM (Kahama), Triple A FM (Arusha) na Jogoo FM (Songea)-(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment