TANGAZO


Saturday, December 20, 2014

Simba yaikung'uta Mwadui ya Shinyanga mabao 3-1 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na timu ya Daraja la Kwanza ya Mwadui ya Shinyanga, wakati wa mchezo wa kirafiki, uliochezwa Uwanja wa Taifa, dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 3-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Golikipa wa timu ya Mwadui, Lucheke Mussa na Ibrahim Twaha wa Simba wakiruka kuuwahi mpira wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Uhuru Selemani wa Mwadui, akikokota mpira baada ya Ibrahim Ajibu kudondoka wakati wakiwania mpira huo.
Joram Mgeveke wa Mwadui (kushoto), akikimbilia mpira na Iddy Bahati wa Simba wakati wa mchezo huo.
Joram Mgeveke wa Mwadui na Iddy Bahati wa Simba, wakiwania mpira, wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Ajibu wa Simba, akitafuta mbinu za kumtoka Joram Mgeveke wa Mwadui ya Shinyanga wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Ajibu wa Simba, akitafuta mbinu za kumtoka Joram Mgeveke wa Mwadui ya Shinyanga wakati wa mchezo huo.
Iddy Bahati wa Simba, akiliruka kwanja la Joram Mgeveke wa Mwadui, wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui ya Shinyanga, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Katika mchezo huo, Simba imeshinda mabao 3-1.
Ahmed Mkweche wa Mwadi, akijaribu kumzuia Iddy Bahati wa Simba, wakati wa mchezo huo.
Ahmed Mkweche wa Mwadi na Iddy Bahati wa Simba, wakiwania mpira wakati wa mchezo huo.
Ubao wa matangazo ukionesha Simba 1, Mwadui 0.
Iddy Bahati wa Simba, akimwacha Ahmed Mkweche wa Mwadi, akiwa amedondoka chini baada ya kumpiga chenga, huku akifuatwa na Salim Khamis wa timu hiyo.
Iddy Bahati wa Simba, akiwania mpira na Salim Khamis wa timu ya Mwadui ya Shinyanga.
Ibrahim Twaha wa Simba akiwapiga chenga mchezaji na golikipa wa Mwadui wakati alipokuwa katika harakati za kuifungia timu yake ya Simba bao la pili katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili la timu yao baada ya Ibrahim Twaha (juu), kuifungia timu yake hiyo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili la timu yao baada ya Ibrahim Twaha (juu), kuifungia timu yake hiyo. Simba imeshinda mabao 3-1.
Hapa ni kipindi cha kwanza Simba ikiongoza kwa mabao 2 na Mwadui bao 1. Hadi mwisho wa mchezo Simba ilishinda mabao 3 dhidi ya bao 1 la Mwadui.

No comments:

Post a Comment