Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, Lanfang Liao, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa tathimini ya mafanikio ya kiutendaji ya kampuni hiyo kwa mwaka 2014 nchini Tanzania. Wa nne kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Jack Yu. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, Lanfang Liao, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, Lanfang Liao, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya StarTimes, Jack Yu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano huo, akielezea kuhusu bidhaa za kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya StarTimes, Jack Yu, akifurahia jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, David Kisaka, akizungumza kuhusu ubora wa bidhaa za kampuni hiyo, wakati wa mkutano huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, David Kisaka, akizungumza na waandishi kuhusu ubora wa bidhaa za kampuni hiyo, wakati wa mkutano huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, David Kisaka, akifafanua jambo kwa waandishi, wakati wa mkutano huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya StarTimes Media, wasambazaji wa ving'amuzi vya luninga vya StarTimes, David Kisaka, akielezea kuhusu simu mpya ya kampuni hiyo ya Solar 5, wakati wa mkutano huo.
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam, Desemba 17, 2014.
OFISI ZA MAKAO MAKUU YA STAR MEDIA
TANZANIA.
Habari za asubuhi ndugu waandishi
wa habari, nawashukuru sana kwa kuitikia wito huu wa kujumuika pamoja nasi
katika hafla hii fupi ikiwa ni maandalizi ya kuumaliza mwaka 2014.
Shukrani
Umekuwa ni mwaka wenye mafanikio
kwa kweli, shukurani za dhati ziwaendee watanzania kwa kuendelea kutuunga mkono
na kutufanya tuendelee kuwa wabunifu zaidi katika huduma na bidhaa tunazozitoa.
Ningependa kutoa shukrani za dhati
kwa vyombo vya habari kwa kazi kubwa mliyoifanya kuhakikisha watanzania
wanapata taarifa sahihi na tena kwa wakati bila
ya kujali umbali waliopo. Tunawashukuru sana na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotulazimu
kuwaita hapa leo na kujumuika nasi kwani uhusuiano wetu ni wa karibu sana ukizingatia
tunategemeana katika kazi zetu za kila siku.
Matawi na maduka ya wakala nchini
Kampuni ya Star Media Tanzania
ambao ndio wasambazaji wa ving’amuzi vya StarTimes ambayo ilianza shughuli zake
mnamo mwaka 2010 kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa
StarTimes imepanua wigo wahuduma zake na kuifikia mikioa 16 ambayo ni pamoja
na; Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Tabora, Bukoba, Kahama,
Morogoro, Mbeya, Iringa, Singida, Musoma, Iringa (DTH), Zanzibar na Songea
(DTH).
Hiyo ni baadhi ya mikoa ambayo
tumekwishaifikia huku mingineyo ikifuata, mikoa yote hiyo ina maduka na
mawakala wanaotoa huduma zetu.
Kutengeneza ajira
Katika dunia hii ya ushindani ajira
ni finyu ambazo huchukua watu wachache sana kulinganisha na uhitaji uliopo.
Kama zilivyo nchi nyingi duniani, serikali ndio muajiri mkubwa, lakini kadri
muda unavyokwenda sekta binafsi imekuwa ikichukua nafasi kubwa katika kuajiri
na kutengeneza ajira kwa watu na hivyo kusaidia serikali kwa kiasi kikubwa.
StarTimes katika shughuli zake
imekuwa ni chachu na ipo mstari wa mbele kuhakikisha inatoa fursa za ajira
mbalimbali iwe za kuajiri moja kwa moja au za watu kujiajiri wenyewe kupitia uwakala.
Baadhi ya watanzania wamenufaika na
uwekezaji wa kampuni hii nchini kwani wengi wao wameajiriwa, ambapo mpaka sasa
kuna wafanyakazi takribani 300 na kampuni imewapa wazawa nafasi nyingi za kazi
na nyadhifa kubwa.
Mbali na ajira za moja kwa moja
kuna wengine wameweza kuchukua fursa ya kuwa mawakala ambapo mpaka kufikia sasa
ndani ya mwaka huu pekee wapo takribani 800 sehemu mbalimbali zilipo huduma
zetu.
Napenda kuwapongeza watanzania kwani
wamekuwa mstari wa mbele kwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazokuja mbele
yao kwa kujiunga kuwa mawakala, wapo waliofungua maduka yanayotoa huduma na
kuuza bidhaa zetu kama vile ving’amuzi, antenna na nyaya zake, simu, runinga,
pamoja na kuuza vocha kwa ajili ya vifurushi vyetu.
Kupitia uwakala huo watu
wanaendesha shughuli zao za kila siku na kulisha familia na kupunguza pengo la
ajira linalotukabili, ni jambo ambalo tunajivunia kwa kweli.
Hivyo basi ni dhahiri uwepo wa
StarTimes nchini umeongeza fursa za uwekezaji, ujasiriamali na hata ushirikiano
kibiashara kwani kuna makampuni kadhaa tunashirikiana nayo katika kutoa huduma
kama vile ya simu na benki.
Kupitia shughuli zote hizi
watanzania wanapata huduma bora na za kisasa, ajira ambazo hukuza vipato vyao
na hata kujiajiri wenyewe, huku nako serikali ikiingiza kodi ambayo inatumika
katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Hii ni dalili nzuri kwamba huduma
na bidhaa zetu ni bora na zinahitajika na watanzania walio wengi. Hivyo basi
kupitia hili tunaamini kwamba tunaiunga mkono serikali yetu katika jitihada za
kupunguza umasikini na kuinua uchumi nchini.
Wateja wetu
StarTimes inajivunia kuwa na wateja
wengi na wanaoongezeka kila kukicha, mpaka sasa tuna wateja zaidi ya 800,000
nchi nzima na hii kuifanya kampuni ya Star Media nchini Tanzania kufanya vizuri
ukilinganisha na matawi ya nchi zingine barani Afrika.
Wateja hawa hatukuwapata kiurahisi
bali ni kutokana na kujizatiti kwetu katika utoaji wa huduma bora ambazo ndio
zimekuwa kipaumbele ukizingatia ushindani mkali uliopo katika soko letu.
Bado kampuni yetu inaimani kubwa
kuwa huduma na bidhaa zake zitaendelea kuwa chaguo la kwanza na tunategemea
kuongeza idadi ya wateja mpaka kufikia mwakani.
Kwa kipindi kifupi tulichowatumikia
watanzania tumejifunza kuwa wanapenda huduma bora na za uhakika, na hicho
ndicho kitu pekee kinachotutofautisha sisi na makampuni mengine yanayotoa
huduma kama sisi.
Na katika kuhakikisha tunawajali na
kuwathamini wateja wetu siku zote tunajitahidi kampuni yetu iwe mstari wa mbele
kutoa huduma bora na kwa bei nafuu ndio maana mnaweza kujionea katika msimu huu
wa sikukuu na shamrashamra za mwaka mpya tumeshusha bei za ving’amuzi vyetu na
kuwaletea ofa kemkem.
Pia kadri siku zinavyokwenda
tunazidi kuwa wabunifu zaidi kwa kuja na chaneli na vipindi mbalimbali ambavyo ni
vyenye manufaa kwa wateja, sio tu kuburudisha bali pia kuelimisha, kufundisha
na kutoa taarifa zenye manufaa kwa maendeleo ya taifa letu changa.
Programu na chaneli zetu
Vinga’muzi vyetu vya antenna za nje
(DTT) pamoja na vya madishi (DTH) vimesheheni channeli na vipindi lukuki zinazo
burudisha, furahisha, kuelimisha na kufundisha kama vile za watoto na katuni,
michezo, filamu, makala, za uchina, za kihindi, habari, tamthiliya, muziki,
wanyama, utafiti, sayansi na teknolojia na nyinginezo nyingi.
Kampuni yetu imekuwa sikivu kwa
wateja wake na tumekuwa tukiwasikiliza wanataka nini, hali hii imepelekea
maboresho ya mara kwa mara ili kuendana na soko la ushindani lililopo sasa.
Ndani ya chaneli hizo, StarTimes
ina dhamira ya dhati kabisa katika kukuza na kuendeleza chaneli za nyumbani
ambazo hutumia lugha ya Kiswahili. Ili Kukuza chaneli hizi na kuzifanya
zipendwe zaidi na watanzania, ving’amuzi vyetu vina chaneli nyingi zaidi za
nyumbani ambazo nyingi ni za bure huku chache zikilipiwa. Mfano wa chaneli
zilizopo ni kama vile TBC1, TBC2, StarTV, ITV, EATV, Clouds TV, TV1, Sibuka
Maisha, CTN, Channel Ten.
Katika jitihada za kukuza lugha ya
Kiswahili, lugha ambayo inakua na kuongelewa sehemu kubwa ya bara la Afrika kwa
sasa, StarTimes imeweka chaneli maalumu ya StarSwahili ambayo vipindi vyake
vyote huruka kwa lugha ya Kiswahili, kuanzia vya nyumbani mpaka vya kigeni
ambavyo vimetafsiriwa kwa lugha hiyo.
Mbali na StarSwahili, pia kuna
chaneli mpya ya Swahili Bollywood, hii ni chaneli inayoonesha filamu za kihindi
ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na hivyo kuwafanya wale wapenzi wa
filamu hizi ambao hawaifahamu lugha hii kupata uelewa na burudani zaidi.
Kwetu sisi tunajisikia fahari na
faraja kubwa sana kuwa sehemu ya kuikuza lugha hii adhimu ya Kiswahili nchini,
barani Afrika na dunia kwa ujumla, pia tunatoa fursa kwa watanzania kuleta kazi
zao na kuweza kupata nafasi ya kurushwa katika cheneli hizi.
Huduma kwa wateja
Kampuni yetu imejizatiti katika
utoaji wa huduma bora kwa wateja ukizingatia wao ndio msingi mkuu wa uwepo sisi
hivyo basi ni lazima kuwatimizia yale wanayoyahitaji.
Huduma kwa wateja imewekezwa kwa
kiasi kikubwa kuhakikisha kwamba mteja anahudumiwa au kufikiwa na huduma zetu
popote pale alipo.
Ufunguzi wa maduka na matawi nchi nzima; Tukianzia
na maduka yetu ambayo yanazidi kufunguliwa kila kukicha nchini, mpaka sasa mkoa
wa Dar es Salaam ambao ndio una wateja wengi zaidi una maduka sita (6) ambayo
yapo maeneo ya; Bamaga-Mikocheni, Mtaa wa Samora-Posta, Buguruni, Tegeta,
Ukonga na Msimbazi-Kariakoo, huku mengine yakipatikana mikoa ya Arusha, Mwanza,
Mbeya, Moshi, Bukoba, Tanga, Iringa, Dodoma na visiwani Zanzibar.
Ufunguzi wa maduka haya unalenga
kuwahudumia vema wateja popote pale walipo na kuwaondolea usumbufu wa kutegemea
duka moja tu. Wingi wa maduka haya unarahisisha huduma zetu, pia unaokoa muda
na gharama za usafiri kwa wateja wetu.
Njia mbalimbali kulipia gharama za vifurushi vya king’amuzi chetu; Zipo njia
nyingi ambazo mteja anaweza kulipia vifurushi, kwa mfano kupitia kwenye ofisi
zetu, kupitia kwa mawakala wetu, njia za huduma za fedha kupitia simu za
mkononi, Selcom na benki. Hii yote ni kumuondolea ule usumbufu wa kusafiri
umbali mrefu, lakini kupitia njia hizi ni kitendo cha dakika chache kabla ya
mteja kuunganisha na kufurahia huduma zetu.
Huduma kwa mteja; StarTimes inayo timu kubwa ya wafanyakazi wanaotoa
huduma kwa wateja wetu kwa njia ya simu, huduma hii hupatikana masaa 24 katika
wiki. Mteja akipiga nambari 0764 700 800 ataweza kuwasiliana moja kwa moja na
kuweza kuhudumiwa kwa chochote kile.
Huduma ya mlango kwa mlango (door-to-door); Huduma hii
inatolewa na mafundi wetu ambao husafiri maeneo tofauti kuhakikisha kwamba
mteja anahudumiwa pale alipo. Kwa mfano pindi mteja anunuapo ving’amuzi vyetu
lakini akashindwa namna ya ufungaji basi mafundi hawa wapo tayari kutoa huduma
hiyo. Pia hutoa msaada wa kiufundi pindi mteja anapopatwa na matatizo katika
ufungaji wake na kupelekea kupata mawimbi hafifu.
Mipango yetu ya baadae
Kama tunavyofahamu Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekwisha tangaza kuwa mpaka kufikia
mwakani mwezi Machi mitambo ya matangazo ya analojia itakuwa imezimwa rasmi na
hivyo kuwalazimu watanzania kuhamia katika mfumo mpya wa dijitali.
Kama StarTimes tumejipanga vema
kuhusu hili na kuwadhibitishia hili mpaka sasa mikoa ya Iringa na Songea tayari
tumekwisha ifikia na huduma zetu na mingineyo ikiwa njiani.
Wateja wetu wanayoimani kubwa juu
ya huduma na bidhaa zetu na kamwe hatuwezi kuwaangusha kwa hilo. Tumekuwa
tukikumbwa na changamoto za kiufundi kuyafikia maeneo ambayo hayana mawimbi
mazuri lakini kuja kwa huduma ya madishi au DTH (Direct-to-Home) tunaamini ni
mombozi mkubwa sana.
Na kwa mujibu wa tathmini
iliyofanyika ndani ya kipindi kifupi tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo mwezi wa
Novemba wateja wengi wameipokea vizuri na wengine kuihitaji mahali waliko.
Kuhitimisha
Lakini kama nilivyosema hapo awali
uwepo wetu sisi kwa watanzania umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana kazi
nzuri mnayoifanya nyinyi na ninaimani kubwa kuwa ushirikiano huu utaendelea
kadri siku zianvyokwenda.
Uongozi wetu siku zetu umeacha
milango wazi kwa maoni, mapendekezo au kupata taarifa zozote ambazo mnaona
zinafaa kufikiwa na watanzania kwa ujumla.
Asante sana kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment