TANGAZO


Wednesday, December 17, 2014

MIKOA 11 YAFANYA VIZURI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na John Banda, Dodoma.
MKOA wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa 11 iliyofanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuongoza katika Wilaya zote 7 kwa asilimia kubwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Khalist Luanda kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Mkurugenzi  huyo  alisema kuwa Mkoa wa Dodoma umekuwa na chanangamoto za kuchanganywa majina na nembo za vyama husika kwenye karatasi, idadi kubwa ya wapiga kura huku kukiwa na msimamizi mmoja kwenye kituo hali iliyofanya watu kukaa sana vituoni na ukosefu wa wino kwa ajili ya kuwawekea alama za vidole waliokwishapiga kura ili kuwaepusha kurudia.

Luanda  alisema hata upigaji wa kura huo ulipositishwa na wahusika kutokana na sababu kama hizo, wananchi walielewa na kusubiri kurudia siku itakayopangwa bila kufanya vurugu zozote.

Kuboja aliitaja Mikoa hiyo iliyofanya vizuria kuwa ni pamoja na Mkoa wa Arusha, Mbeya, Kagera, Njombe, Singida, Lindi, Ruvuma, Katavi, Geita, Iringa na Mtwara.

Aidha Luanda alisema katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi kwa asilimia kubwa katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma huku wakifuatiwa na CHADEMA na CUF.

CCM imepata vijiji 7,290 kati ya vijiji 9,290 vilivyotoa matokeo
Uchaguzi Serikali za Mitaa


Na Joyce Kasiki, Dodoma
KATIKA uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka huu, matokeo ya jumla yanaonesha Chama cha Mapinduzi kimepata ushindi kwa kupata vijiji 7,290 Kati ya vijiji 9,290 vilivyotoa matokeo.

Kauli hiyo ilitolewa Jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Khalisti Luanda wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini hapa.

Alisema,katika matokeo hayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimepata vijiji 1,248,TLP vijiji viwili,NLD viwili,na UDP vijiji vinne na CUF ilipata vijiji 949.

Akitoa matokeo ya Mitaa,Khalisti alisema ,Kati ya Mitaa 3,078 ilitoa matokeo ,CCM imepata Mitaa 2,116,Chadema Mitaa 753,
CUF Mitaa 233,NCCR-Mageuzi Mitaa minane,TLP Mtaa mmoja na ACT Mitaa tisa

Vyama vingine ni UMD Mtaa mmoja,UDP Mtaa mmoja,na NRA Mtaa mmoja.
Aidha Khalisti alisema,mwisho wa kutoa matokeo kwa maeneo yote yaliyofanya uchaguzi Desemba 14 mwaka huu ni kesho (leo).

Mkurugenzi huyo pia amesema katika mchakato huo wa uchaguzi mikoa 11 imefanya vizuri.
Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha, Dodoma, Mbeya,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Katavi,kagera,Iringa na Njombe.

Pia ameitaja mikoa iliyofanya vibaya ambapo amesema ni mikoa ya Kigoma,Tabora,Pwani.

No comments:

Post a Comment