Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe, akitoa tamko, Dar es Salaam leo, kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dk. Ayoub Magimba. (Picha zote na Magreth Kinabo, Maelezo)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (kulia), akitoa tamko, Dar es Salaam leo, kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dk. Ayoub Magimba.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (kulia), akifafanua jambo, wakati alipokuwa akitoa tamko, Dar es Salaam leo, kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dk. Ayoub Magimba.
Naibu Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen
Kebwe (kulia), akifafanua jambo, wakati alipokuwa akitoa tamko, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dk. Ayoub
Magimba.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. Sijenunu
Aaron (kushoto) na Mratibu wa Kisukari wizarani hapo, Dk.Auson
Rwehumbize wakiwa kwenye mkutano huo.
"Hii
picha ni lazima niipate" ni kama anaongea Halima Kambi mpiga picha wa
Kampuni ya The Guardian Limited wakati Naibu Waziri Kebwe Stephen
alipokuwa akitoa tamko hilo kwa wanahabari.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Na
Beatrice Lyimo- Maelezo
SERIKALI
imetoa wito kwa kila mwananchi nchini kuhakikisha kwamba anapima afya yake mara kwa mara
kwa kuwa ugonjwa wa kisukari unaweza usionyeshe dalili yoyote mapema ili
kuweza kukabiliana na kupunguza athari
za ugonjwa huo
Aidha
Serikali imesisitiza kuwa endapo mtu atatambulika kuwa ana ugonjwa huo, atumie huduma za afya
kulingana na ushauri wa atakaopewa na wataalam wa afya.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Stephen Kebwe
leo alipokuwa anatoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa
Novemba 14, mwaka huu duniani kote yenye kauli mbiu “Ulaji unaofaa, huanza na
mlo wa asubuhi”.
Siku
ya kisukari duniani ilianzishwa baada ya kuona ugonjwa wa kisukari unaongezeka
sana duniani kote na Tanzania kama nchi nyingine duniani huadhimisha siku hii kwa
kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na
kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huu, alisema Naimu
Waziri.
“Ugonjwa
wa Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi
kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu” aliongeza Dkt Kebwe.
Amebainisha
kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania, na tafiti zinaonyseha kuwa mwaka 2007 kulikuwa
na wagonjwa 246 milioni duniani,mwaka 2012 wagonjwa milioni 371, mwaka 2013
wagonjwa milioni 382ulimwenguni kote na
mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa milioni 19.8 barani Afrika.
Aidha
nchini Tanzania kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha
wilaya 50 ulionyesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na
kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.
Dk. Kebwe
aliongeza kuwa takwimu za watoto wenye kisukari mwaka huu ni kati ya
asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki za
hapa nchini.
“Lakini
wapo wengine hawajitokezi kwenye kliniki kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani
potofu, gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilizopo” aliongeza Naibu
Waziri huyo.
Aidha
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na utekelezaji wa
Sera ya Afya(2007) inayolenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo
kisukari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani ya Nchi na wa kimataifa.
Tanzania
inaungana na mataifa yote duniani kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la
mwaka 2011 la kuhakikisha magonjwa yasio ya kuambukiza yanapungua kwa asilimia
25 ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment