TANGAZO


Wednesday, November 19, 2014

Wafanyabiashara ndogondogo wafanya vurugu kupinga kuondolewa kwa nguvu katika maeneo yao jijini Mwanza leo

Askari akimwamrisha mwananchi akae chini  aliyekuwa akipita katika eneo la tukio kufuatiaVurugu zilizokuwa zikiendelea kati ya askari na Wafanya Biashara ndogondogo kuondolewa kwa nguvu
 jijini Mwanza  leo kwa madai ya kipande cha  Mtaa wa Makoroboi kupewa Mwahindi wamiliki kipande hicho, kipande hicho kimepewa  jina la Pramukh Swami ST(PICHA NA KHAMISI MUSSA)

Wafanya kazi wa Benki ya Accss Benk Jijini Mwanza wakiingia ndani ya Jengo hilo Barabara ya Nyerere baada ya kuzidiwa na mvuke wa mioshi ya Mabomu hayo leo.
Wafanya kazi wa Benki ya Accss Benk Jijini Mwanza wakiingia ndani ya Jengo hilo Barabara ya Nyerere baada ya kuzidiwa na mvuke wa mioshi ya Mabomu hayo leo.
Wananchi wakiwa wamepakiwa katika Gari la Polisi jijini Mwanza kufuatia vurugu hizo.
Askari wa FFU, wakimdhibiti kijana aliyekuwa akisukuma toroli la kubebea mizigo.
Dereva wa Pikipiki ya kubebea mizigo yenye namba za Usajili T594 AWG, akisaidiwa na wananchi kusukuma KWA kujisalimisha baadaya kuzimika kufuatia vurugu za Askari na wafanya biashara Ndogondogo katika Kipande cha Mtaa wa Makoroboi kuondolewa kwa nguvu.
Askari wa FFU,wakishauriana wakati walipokuwa wakidhibiti vurugu hizo.
Wafanya Biashara na Wananchi wakikimbia wakiwa katika Barabara ya Rwagasore na Mtaa wa Maket jijini Mwanza leo.
Askari wa FFU, wakimuongoza kijana baada ya kumdhibiti katika vurugu hizo.

Maelezo mafupi kuhusu sakata hilo.
Wafanya Biashara Ndogondogo (Wamachinga) wamefukuzwa na Askari wakishirikiana na Askari wa Jiji la Mwanza kuwaondoa  eneo walilokuwa wakifanyia Biashara zao,
 ambalo walidai Eneo hilo wanafanya Biashara zao kwa Muda wa Miaka mingi na wanaishangaa serekari kwakutumia nguvu nyingi ya bila ushirikishwaji , hata hivyo mwananchi ambaye hakutaka jina lake kutotajwa
Gazetini ,ametoa tuhumwa kwa Mkuu wa kituo Kidogo cha Polisi Makoroboi na Kituo kidogo cha Nyamagana kuwa chanzo cha Vurugu hizo na Maduka kufungwa pamoja na kituo cha Daladala kutotumika na wananchi wakihangaika kwa
kusaka usafiri kutokana vurugu hizo. Sehemu ya kieneo cha  Mtaa wa Makoroboi umepewa jina la Pramukh Swami, ambapo wamiliko ni Wahindi.


No comments:

Post a Comment