*Awaambia wana-CCM: Serikali inashughulikia matatizo yanayowakabili
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akipokea taarifa ya chama Wilaya ya Amani kutoka kwa Katibu, Abdalla Mwinyi (kulia) wakati wa mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Mjini, Unguja, wakati akiwa katika ziara ya kuimarisha chama hicho mikoa ya Unguja leo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai. (Picha zote na Ikulu)Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Mjini Mhe. Borafya Silima Juma akiwapa nasaha Mabalozi wa CCM Mkoa wa Mjini katika wilaya ya Amani wakati mkutano wa kuimarisha Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni mfululizo wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Mjumbe wa Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani CCM kutoka Mpendae Gabriel Mlekwa akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja.
Balozi kutoka Shehia ya Kwawazee jimbo la Magomeni Juma Ameir Jecha akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja
Balozi kutoka Shehia ya Chumbuni Bibi Nunuu Khatib Hamad akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi wa Majimbo mbali mbali ya wilaya ya Amani Unguja akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani leo.
Na Said Ameir, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakishia wananchi
kuwa Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa matatizo mbalimbali yanayowakabili
yanapatiwa ufumbuzi kwa wakati kulingana na mipango na uwezo wa serikali.
“hatushabikii maovu
wala matatizo ya wananchi. Serikali kwa ujumla wake inachukua hatua mbalimbali
na kupanga mipango madhubuti kuona matatizo hayo yanapatiwa ufumbuzi” Dk. Shein
alisisitiza.
Akizungumza na mabalozi
wa nyumba kumi na viongozi wa Maskani za Chama cha Mapinduzi wilaya ya kichama
ya Amani mjini Unguja leo, Dk. Shein amesema ni bahati mbaya kuona kuwa wakati
mwingine baadhi ya wanasiasa wanajaribu kuyaeleza matatizo hayo kuwa ni mambo
madogo yanayoweza kuondolewa mara moja.
“Kwa mfano suala la
ajira si jambo dogo kama baadhi ya watu wanavyojaribu kulieleza kwa wananchi ili
kujipatia manufaa ya kisiasa. Hii inanitia shaka kwa kiongozi kufanya jambo
hilo” Dk. Shein alieleza.
Alifafanua kuwa ajira
si tatizo la Zanzibar pekee bali duniani kote na kutoa takwimu zikionesha kuwa tatizo
hilo kwa sasa Zanzibar limefikia asilimia 17 ya watu wote na kati ya hao vijana
ni asilimia 14.
“Ningependa kuona vijana wote na wananchi wa Zanzibar
wana ajira lakini sisi hatujawa na uwekezaji mkubwa wa kutoa ajira nyingi wala
ardhi kubwa ya kukidhi mahitaji ya ajira kwa watu wetu” Dk. Shein aliongeza.
Kwa hivyo aliwaeleza
kuwa ndio maana Serikali imeamua kuwahamasisha vijana wanaomaliza masomo yao
pamoja na makundi mengine kujiajiri na serikali kwa kushirikiana na washirika wa
maendeleo kuwawezesha ili kumudu kujiajiri.
Tatizo la ajira
pamoja na huduma zisizoridhisha katika Hospitali Kuu ya Mnanzi mmoja ni
miongoni mwa masuala yaliyogusiwa na viongozi waliopata fursa ya kutoa maoni yao
ambapo Mhehimiwa Rais alitumia fursa hiyo kuyatolea ufafanuzi baadhi yake.
Kuhusu huduma katika
hospitali hiyo kuu iliyopo mjini Unguja, Dk. Shein aliwahakikishia kuwa taarifa
ya baadhi ya mapungufu anazo na anafuatilia kwa karibu suala la uimarishaji wa
huduma katika hospitali hiyo na nyingine humu nchini.
Alifafanua kuwa hivi
sasa kuna hatua nyingi zinazochukuliwa katika kuimarisha hospitali hiyo kwa
kushirikiana na washirika wa maendeleo na hatua hizo ni katika kutekeleza azma
ya serikali kuimarisha huduma za rufaa katika hospitali hiyo.
Kuhusu utelekezaji wa
agizo lake la kutaka wajawazito wasitozwe fedha wakati wa kujifungua iwe kwa njia
ya kawaida au kwa upasuaji, Dk. Shein alisema lipo tatizo la kutotekelezwa kikamilifu
agizo hilo lakini alifafanua kuwa hali hiyo wakati mwingine inatokana na wizara
ya Afya kutopata fedha za matumizi mapema lakini pia wakati mwingine ni matatizo
ya baadhi ya watumishi wa afya.
Kwa hivyo aliwaahidi
kuendelea kufuatilia suala hilo na mengine ambayo viongozi hao walimueleza
wakati wa kutoa maoni yao.
“Serikali yenu ni
sikivu, lazima tuzingatia maoni yenu na hoja zenu kwani ni za msingi hivyo
tunahitaji kuzitafakari na kuzifanyia kazi kwa kuwa tunapaswa kuzijibu kwa
umakini ” Dk. Shein aliwaambia viongozi hao.
Katika mkutano huo,
Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar,
aliwataka wana CCM kuendelea kushirikiana na Serikali katika kupambana na maovu
katika jamii ikiwemo vitendo vya udhalilishaji
wa watoto na wanawake na kwamba yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kuvikemea
vitendo hivyo kila anapopata fursa ya kufanya hivyo.
Mapema Mwenyekiti wa
CCM wilaya hiyo ya kichama ya Amani Abdi Ali Mzee mbali ya kumpongeza Mheshimiwa
Rais kwa kusimammia vyema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa lakini pia alitoa
wito kwa Mawaziri kwenda kwa wananchi kuwaeleza mafanikio mbalimbali
yaliyopatikana na katika kutekeleza mipango ya maendeleo.
“Tunaomba shughuli za
utekelezaji wa Ilani zitangazwe na kuoneshwa katika televisheni na vyombo
vingine vya habari ili wananchi waweze kuelewa ili kuepuka upotoshaji ambao
umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu” alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, aliwaambia viongozi hao kuwa Katiba
iliyopendekwa si ya Chama cha Mapinduzi kama baadhi ya watu wanavyoeleza bali ni
ya wananchi wote wa Zanzibar kwani wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
waliopitisha kwa theluthi mbili kutoka Zanzibar wametoka katika makundi yote.
“Tuwapongeze wabunge
hao kwa ujasiri wao na kutetea maslahi ya Zanzibar katika Katiba iliyopendekezwa
” alisema Bwana Vuai.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu
pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
No comments:
Post a Comment