TANGAZO


Friday, November 14, 2014

Viongozi wa Kampuni ya Star Times watembelea Kampuni ya Jambo Leo katika kuimarisha uhusiano wa kikazi

Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto), akionyeshwa magazeti yanayochapishwa na Jambo Leo Publications wakati alipotembelea kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi katika ofisi zao, zilizopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Anicetus Busagi Mwesa.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto), akipatiwa ufafanuzi na Mhariri wa Habari, Bw. Said Mwinshehe juu ya shughuli za kiuandishi za magazeti yanayochapishwa na Jambo Leo Publications wakati alipotembelea kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi katika ofisi zao, zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (wa kwanza kulia), akipatiwa ufafanuzi na mwandishi wa habari, Peter Ambilikile juu ya shughuli za kiuandishi za magazeti yanayochapishwa na Jambo Leo Publications wakati alipotembelea kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi katika ofisi zao, zilizopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Anicetus Busagi Mwesa.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto), akipatiwa ufafanuzi na Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Anicetus Busagi Mwesa juu ya shughuli za uhakiki wa gazeti unaofanywa na Bw. J. Mabula (kulia aliyekaa), wakati alipotembelea ofisi za Jambo Leo Publications kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia), akiteta jambo na Meneja Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Bw. Ramadhan Kibanike, wakati alipotembelea ofisi za gazeti hilo, kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (wa kwanza kushoto), akipeana mkono na mwandishi wa habari Grace Gurisha, wakati alipotembelea ofisi za Jambo Leo Publications kujionea shughuli na pia kujenga mahusiano ya kikazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Anicetus Busagi Mwesa.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (wa kwanza kushoto), akipata ufafanuzi kutoka kuhusu Jarida la Jambo Brand kutoka kwa Mhariri wa Jarida hilo, Bw. Erick Toroka (kulia), ambalo huandaliwa na gazeti la Jambo Leo. Katikati ni Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Anicetus Busagi Mwesa. (Picha zote na Kijanga Geofrey wa Star Times)

No comments:

Post a Comment