Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akisalimiana na Viongozi, wakiwemo
wawekezaji wa Kampuni na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na
Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”, uliofanyika
leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani, Mjini Unguja. (Picha zote na Ikulu)
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein
akisalimiana na Viongozi wa mbali mbali
wakati wa uzinduzi wa
Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth
Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa
Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akizungumza na Waziri wa Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman kabla ya uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi wa Idara za Serikali ya Mapinduzi walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein alipozungumzanao leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein alipozungumzanao leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Taki Dewji wa banda la Shell wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Rose Tesha Meneja Vipindi katika banda la VSO wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipatiwa maelezo wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipatiwa maelezo wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipatiwa maelezo wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamd Shein akipatiwa maelezo wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamd Shein, akizungumza wakati akilizindua Tamasha la Vijana, Hoteli ya Bwawani, mjini Unguja leo.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar
imekuwa ikichukua juhudi mbali mbali zinazolenga kujenga mazingira
yatakayowawezesha vijana kuimarisha fursa za ajira ikiwa ni utekelezaji wa mipango
mikuu ya maendeleo pamoja na kuridhia na kutekeleza mipango inayoendelea
kupangwa na taasisi za Kimataifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa maonyesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji
kwa Vijana, yaliyofanyika huko katika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Serikali imekuwa ikisiamamia
utekelezaji wa Sera ya Ajira ya Zanzibar ambayo inatilia mkazo suala la
kuwashajiisha vijana kujiajiri wenyewe na kujenga mazingira mazuri ili vijana
wanawake na wanaume wapatiwe nyezo muhimu za kuansiha na kuimarisha biashara na
shughuli nyengine za kuendesha maisha yao.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imelipa kipaumbele
suala la maendeleo ya vijana, ikiwemo suala zima la uimarishaji wa fursa za
ajira, ili nguvu kazi ya taifa iweze kutumika vyema katika kuleta maendeleo ya
kiuchumi na kijamii.
“Serikali ya Mmapinduzi Zanzibar katika awamu zake zote tangu
yaliopofanyika Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, imekuwa
ikizingatia sana suala la maendeleo ya vijana na nafasi katika jamii... Awamu
ya saba, imekuwa ikipanga na kutekeleza mipango mbali mbali yenye lengo la
kuimarisha ystawi na fursa za vijana”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa serikali imechukua hatua za kuansiha mifuko
mbali mbali kwa lengo la kupata fedha na kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri
wenyewe ambapo imeanzisha Mfuko wa uwezeshaji ambao aliuzindua tarehe 21
Decemba, 2013 na tayari vikundi mbali mbali vya Unguja na Pemba vimeanza kupata
mikopo.
Dk. Shein aliwafahamisha vijana na
wananchi kuwa Serikali inaendelea kutafuta njia bora za kuimarisha mafunzo ya
amali pamoja na kuhamasisha mabadiliko katika Sera ya Elimu kwa lengo la
kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inawaongoza vijana katika ubunifu wa mbinu
bora za kujiajiri wenyewe.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Serikali itachukua hatua za
maandalizi ya awali katika kutafuta uwezekano wa kuchimba mafuta hapa Zanzibar
na vijana wana fursa nzuri ya kunufaika na ajira mbali mbali zitakazokuwepo na
kueleza hatua zilizofikiwa juu ya suala hilo.
Alieleza kuwa kwa kutambua mahitaji ya utaalamu na nguvu kazi inayohitajika
katika sekta ya mafuta na gesi, jambo la kwanza la kulifanyia kazi ni kuanza
kuwatayarisha vijana, ili wakati utakapowadia wawe mstari wa mbele katika
kuitumikia na kuiongoza sekta hiyo.
Dk. Shein alisisitiza kuwa katika Makubaliano ya Awali waliyotiliana saini
na Kampunin ya SHELL kutoka Uholanzi ni kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na
mfupi vijana wa Kizanzibari ili kujenga nguvu kazi iliyopo yenye utaalamu na
maarifa yanayokwenda sambamba na
mahitaji ya sekta hiyo na mipango ya nchi ambapo tayari vijana 19
wanasomea fani ya mafuta na gesi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa
ushauri kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali
kwa kuonesha uzalendo na ari ya kujifunza mambo mbali mbali wanayotayarishiwa
na Serikali yao.
Aidha, alisema kuwa maonyesho hayo ni miongoni mwa mikakati ya Serikali ya
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana na kuona fursa zilizopo hasa wakati
huu ambapo tatizo la ajira kwa vijana limekuwa ni changamoto kubwa kwa takriban
Serikali za nchi zote duniani.
Alisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaonekana kuwa kubwa
zaidi kwani kwa mujibu wa utafiti huo, Zanzibar inakisiwa kuwa na asilimia 17
hadi 18 ya vijana wenyewe umri kati ya miaka 15-24 wasiokuwa na ajira ambapo
pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwataka vijana kutochagua kazi.
Aliwasihi vijana kutofuata mambo mabaya wala wasishawishiwe kuingia katika
mambo hayo maovu na badala yake washawishike kuingia kwenye mambo mazuri ikiwa
ni pamoja na kutafuta njia za kuweza kujiajiri, kuwa na busara kwani
wanahitajika kuanza familia zao huku akiwasisitiza kuisikiliza serikali yao.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa taasisi taasisi zote za
serikali na binafsi zilizohusika pamoja na Shirika la Huduma za Kujitolea (VSO)
kwa kazi kubwa ya kufanikisha maonyesho hayo, pia alitoa pongezi kwa Shirika la
SHELL kwa kuiunga mkono Zanzibar.
Mapema Dk. Shein alikagua maonyesho yalioandaliwa kwa mantiki ya kuonesha
fursa za ajira na uzalishaji kwa vijana na kupata maelezo kutoka kwa wahusika
ambapo nae alitumia fursa hiyo kupongeza kutokana na juhudi zao hizo sambamba
na ushiriki wao mkubwa.
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali
Suleiman kwa niaba ya Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na
Watoto alisema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2020
sambamba na kukuza uchumi na kupunguza umasikini MKUZA huku akieleza umuhimu wa vijana katika jamii.
Nae Mwenyekiti wa Shirika la SHELL International Bwana Axel Knospe na Mkurugenzi Mkaazi wa VSO
Bwana Jean Van Wetter walitumia fursa hiyo kutoa pongezi kutokana na juhudi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kupambana na tatizo la ajira kwa vijana
huku wakiahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Nao vijana wakitoa neno lao la shukurani walipongeza juhudi za Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Shein pamoja na nasaha zake
alizowapa sambamba na juhudi za Serikali katika uwezeshaji na uimarishaji wa
ajira kwa vijana, kuwepo kwa Baraza la Vijana, huduma rafiki kwa vijana na
uimarishaji na upatikanaji wa elimu ya juu na vyuo vya amali.
Dk. Shein pia alikabidhiwa Ripoti ya Idadi ya watu duniani na Dk. Lutosho
Dadi kutoka UNFPA ambapo kabla ya kumkabidhi Dk. Dadi alieleza kuwa hivi sasa
vijana wameweza kufikia Bilioni 1.3 duniani ambapo kwa upande wa Zanzibar Sensa
ya mwaka 2012 ilionesha kuwa vijana wa Zanzibar ni asilimia 77 chini ya umri wa
miaka 35 na kueleza kuwa juhudi za makusudi zinahitajika katika kuwaletea
maendeleo vijana.
Viongozi mbali mbali walihudhuria katika maonyesho hayo, akiwemo Spika wa
Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mawaziri mbali mbali, Makatibu
Wakuu,Wawakilishi wa Mashirika ya Maendeleo pamoja na vijana na wananchi na
wajasiria mali mbali mbali.
No comments:
Post a Comment