TANGAZO


Friday, November 28, 2014

Rais Dk. Shein awaapisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu, Ikulu mjini Zanzibar

Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali wakifuatilia kwa makini walipokuwa wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha zote na Ikulu)
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati)akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa wakifuatilia kwa makini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwwapisha Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali na Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Hassan Said (kulia) akiwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika Viapo mbali mbali vya Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu wa Serikali waliapishwa leo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali wakifuatilia kwa makini walipokuwa wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Khamis Jabir Makame  kuwa Mkuu  wa Wilaya ya Kusini Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Haji Makungu Mgongo  kuwa  Mkuu  wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Hassan Khatib Hassan kuwa  Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Khadija Bakari Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi Madina Mjaka Mwinyi kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Said Seif Mzee kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Juma Yakout Juma kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi mbali mbali katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Viongozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Bwana Khamis Jabir Makame ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja ambapo kabla ya uteuzi wake huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja,  Luteni Kanali Mstaafu Haji Makungu Mgongo ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja ambapo kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja.
Bwana Hassan Khatib Hassan ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, Bibi Khadija Bakari Juma ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bibi Madina Mjaka Mwinyi ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Wengine ni Dk. Said Seif Mzee ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Dk. Juma Yakout Juma, ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo  baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Kasim Tindwa, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

No comments:

Post a Comment