TANGAZO


Monday, November 24, 2014

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal afungua mkutano wa Kitaifa wa Taasisi za Fedha AICC jijini Arusha leo

Washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji wa Sekta ya kilimo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua mkutano huo leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo, mkutano huo ulifanyika leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano  wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo leo    Novemba 23-2014 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.   
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Edwin Mtei nje ya ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha leo Novemba 23-2014 baada ya kufungua mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji wa sekta ya kilimo. (Picha zote na OMR)

No comments:

Post a Comment