Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimtukuku Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo Amina Salum Mwanja wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga akitoa neno baada ya Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kumaliza shudhuli ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesomea Shahada ya kwanza ya Mipango ya Usimamizi wa Mazingira katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Azizi Mshau akimweleza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene namna bora ya kundaa mipango miji inayokuwa rafiki kwa mazingira.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akiagana na Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga mara baada ya sherehe ya mahafali ya 28 ya Chuo hicho.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene () akiwa katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) mara baada ya mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Dodoma)
Na Eleuteri Mangi-
Dodoma
Serikali imesema inaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuweka
mazingira rafiki kwa kuboresha mifumo ya ajira katika sekta ya umma na ile ya
binafsi ili kujenga uchumi wa kisasa unaozalisha ajira pamoja na kuwawezesha
vijana wasomi nchini kujiajiri.
Kauli hiyo imetolewa na
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kwa niaba ya Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini
(IRDP) yaliyofanyika jana mjini Dodoma.
“Ninafarijika sana
kusikia vijana wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini wameweza kuonesha njia
kwa kuweka kwa vitendo waliyojifunza kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi katika
sekta ya kilimo kama njia ya kujiajiri” alisema Mbene.
Naibu Waziri huyo aliwahakikishia
vijana hao kuwa Serikali ipo tayari kusaidia juhudi hizo kupitia fursa
mbalimbali za kuwasaidia vijana na wajasiriamali kupitia fursa zinazoendelea
kutolewa na Serikali.
Naibu Waziri Mbene
alisema kuwa ili kutekeleza lengo hilo, Serikali inaendelea kuhamasisha
uwekezaji katika kilimo, uchimbaji wa madini na uwezo wa kuongeza thamani mazao
yetu yanayozalishwa.
Mbene aliongeza kuwa
maeneo yote hayo yanatoa fursa nyingi kwa wahitimu vijana nchini kuajiriwa
katika ngazi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na kujiajiri.
Akimkaribisha Mgeni
rasmi kwenye mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Dkt. Razack
Lokina alitoa kilio cha chuo hicho cha kuomba kada ya mipango kupewa nafasi
stahili katika mfumo wa ajira Serikalini.
Akifafanua suala hilo Dkt.
Razack alisema kuwa kukosekana kwa kada ya Mipango kumesababisha kazi za kada
hiyo kutotekelezwa ipasavyo kwa kiwango cha ufanisi unaotakiwa.
Aidha, Dkt. Razack
alisema kuwa taaluma ya Mipango inamtayarisha Afisa Mipango ambaye jukumu lake
ni kubuni, kupanga, kufuatilia, kutathmini, kuratibu shughuli na rasilimali
katika maeneo ya Mipango ili kufikia malengo ya maendeleo ya jamii kusudiwa tofauti
na taaluma ya Uchumi ambayo inamuandaa Afisa kuwa na jukumu mahususi la
kuchambua ili kutoa hali halisi ya mazingira ya kiuchumi kisekta.
Kwa upande wake Chuo
hicho Constantine Lifuliro alisema kuwa wahitimu wa chuo chake wameandaliwa vya
kutosha wapo tayari kutoa huduma katika nyanja mbalimbali kwenye maeneo
waliyojifunza hasa katika kuandaa, kusimamia, kutekeleza, kufuatilia na
kutathmini mipango ya maendeleo katika maeneo mbalimbali watakayofanyia kazi.
Naye mhitimu Baltazar
Ngeze, kwa niaba ya wahitimu wa mwaka huu wa chuo hicho aliushukuru uongozi wa
chuo kwa kuwaandaa vema kwenda kutekeleza majukumu yao ya taaluma ya Mipango
katika jamii watakayokuwepo.
Katika mahafali hayo jumla
ya wahitimu 1,909 waliotunukiwa tuzo zao katika kozi mbalimbali zinazotolewa
chuoni hapo.
Kati ya wahitimu hao,
wapo wanaume ambao idadi yao ni 1,003 sawa na asilimia 52 ya wahitimu wote na
wanawake idadi yao ikiwa ni 906 sawa na asilimia 48 ya wahitimu wote.
Idadi hiyo ya wahitimu
wa mwaka huu inaonesha wameongezeka wahitimu 63 sawa na silimia 3.4 zaidi ya
wale waliohitimu masomo yao mwaka jana 2012/2013 ambao walikuwa 1,846 kati yao
wakiwa wanaume 1,037 sawa na asilimia 56 na wanawake walikuwa 809 sawa na
asilimia 44.
No comments:
Post a Comment