TANGAZO


Sunday, November 30, 2014

Bashir ataka UN-AU waondoke Darfur

Askari wa kuweka amani Darfur
Rais wa Sudan ametaka vikosi vya kimataifa vya kuweka amani vitayarishe mpango wa kuondoka Darfur, miaka saba tangu vikosi kupelekwa huko.
Rais Omar al-Bashir alisema wanajeshi wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hawawezi hata kujilinda wenyewe.
Aliwaambia waandishi wa habari mjini Khartoum kwamba askari hao wa kuweka amani wanawalinda wapiganaji badala ya raia.
Serikali ya Rais Bashir imechafua juhudi za askari wa amani kuchunguza tuhuma za ubakaji unaofanywa na wanajeshi wa Sudan huko Darfur.

No comments:

Post a Comment