Diwani wa Kata ya Nzuguni Chiwanga Magongo, akizungumza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Dkt. David Malole.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Dkt. David Malole akifafanua jambo mbele ya wananchi wa Kata ya Nzuguni, iliyopo Manispaa ya Dodoma wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Daladala kwa Masista.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, akitoa maelekezo kwa mmoja wa akina mama wanafanya biashara ya nyanya na mbogamboga katika stendi ya Daladala ya kwa Masista, Nzuguni Manispaa ya Dodoma mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, akitoa maelekezo kwa mmoja wa akina mama wanaofanya biashara ya nyanya na mbogamboga katika stendi ya Daladala ya kwa Masista, Nzuguni Manispaa ya Dodoma mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa Mipango Miji na Mazingira wa Manispaa ya Dodoma, Msinta Mayaoyao, akielezea jambo mbele ya wananchi wa Kata ya Nzuguni alipokuwa akiwatoa hofu ya kutopimiwa viwanja vya makazi huku kukiwa na tishio la kuvunjiwa nyumba zao.
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nzuguni akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Dkt David Malole baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kimila wa kabila la Kigogo wa Kata ya Nzuguni kutokana na kuwatetea wakazi wa Manispaa ya Dodoma katika suala la Ardhi.
Mkazi wa Nzuguni, Manispaa ya Dodoma, John Sawasawa akiuliza swali mbele ya Mbunge David Malole kuhusiana na viongozi wa Kata ya Nzuguni kudaiwa kuvitenga vitongoji vitano vya Kawawa, Karume, Misheni, Shule ya Msingi Nzuguni A' na Sokoine kwa kutowapelekea miradi ya maendeleo ikiwemo umeme na maji.
Wananchi wa Kata ya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbambali za viongozi waliohudhuria mkutano wa hadhara, uliohudhuriwa na Mbunge wa imbo la Dodoma mjini Dkt David Mchiwa Malole anaendelea na ziara katika kata zote za manispaa hiyo.
Wananchi wa Kata ya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma, wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbambali za viongozi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Dkt David Mchiwa Malole, anaendelea na ziara katika kata zote za manispaa hiyo. (Picha zote na John Banda-Dodoma)
No comments:
Post a Comment