TANGAZO


Wednesday, October 15, 2014

Mkutano wa siku mbili wa kujadili Sekta ya Mawasiliano Afrika Mashariki na Kati na Afrika kijumla wafanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kushoto), akiteta jambo na Meneja Biashara wa Kampuni ya CSg, Hamza Zamouche mara baada ya kuufungua Mkutano wa siku mbili wa kujadili Sekta ya Mawasiliano Afrika Mashariki na Kati na Afrika kijumla, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Safari Com ya Kenya akiwasilisha mada kuhusu utendaji kazi wa masuala ya kifedha ya mtandao huo, ujulikanao kama M Kopa.
Meza Kuu wakitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya mtandao wa mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na Afrika kijumla. Kulia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu Serikali inavyoweza kuwasaidia wawekezaji katika miradi ya mawasiliano kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya TelServ (aliyekaa), Vincent Peek, akimpatia mteja maelezo kuhusu kampuni hiyo pamoja na utendaji kazi wake.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kulia), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuufungua mkutano huo jijini leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (wapili kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. 
 Ofisa wa Kampuni ya TTCL, akifafanua jambo kwa waandishi wakati wa mkutano huo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya TelServ (aliyekaa), Vincent Peek, akiwapatia wateja waliotembelea kwenye banda la kampuni hiyo, maelezo kuhusu kampuni pamoja na utendaji wake wa kazi.
Maofisa wa Kampuni ya simu ya Vodacom, wakiwapatia maelezo wageni waliotembelea kwenye banda la kampuni hiyo.
Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo, wakiwa katika majadiliano na wageni mbalimbali waliowatembelea.
Maofisa wa Shirika la Simu la Namibia wakiwa kwenye banda la shirika hilo, wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Simu ya Six Telecoms, Rashid Shamte, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni yake hiyo. 
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kushoto), akipatiwa maelezo na Mratibu wa Mambo ya Ufundi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), Mhandisi Anifa Chingumbe, kuhusu utendaji kazi wa mkongo huo, wakati alipotembelea banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), baada ya kuufungua Mkutano wa siku mbili wa kujadili Sekta ya Mawasiliano Afrika Mashariki na Kati na Afrika kijumla, Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kushoto), akiagana na Mratibu wa Mambo ya Ufundi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), Mhandisi Anifa Chingumbe, mara baada ya kupatiwa maelezo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya Mawasiliano wa TM, Bhavin Shah (katikati), akimpatia maelezo mmoja wa wageni waliotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mkutano huo.
Msaidizi Binafsi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya WiA, ManPreet Chana akionesha nembo ya kampuni hiyo kwa wageni waliotembelea kwenye banda la kampuni hiyo, wakati wa mkutano huo jijini Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment