Monday, October 6, 2014
Washindi wa Mbio za Baiskeli za Shimiwi watunukiwa medali
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka Hazina, Prisca Kahimba (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka RAS Pwani, Agatha Gambi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka Uchukuzi Johari Moshi akimalizia mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro jana.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka Uchukuzi, Johari Moshi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Utumishi Hassan Ligoneko akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro jana.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Utumishi, Hassan Ligoneko (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka RAS Tanga, Ezekiel Mhina (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Ikulu John Fataki akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Ikulu, John Fataki (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro jana. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Polisi wa usalama barabarani akizuia magari kabla ya kuanza kwa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 katika mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro jana.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 kutoka Uchukuzi Johari Moshi (kulia) akijaribu kuwapita washiriki wenzake katika mashindano ya mbio za baiskeli ya SHIMIWI mjini Morogoro jana.
Baadhi ya watumishi wa Serikali kutoka Wizara,Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali wakisubiri msafara wa mbio za baiskeli za wanawake kuwasili katika kituo cha Lake Oil mjini Morogoro jana.
Watumishi wa Hazina wakishangilia baada ya mchezaji wao kuwasili kituo cha mwisho cha mbio za baiskeli cha Lake Oil mjini Morogoro jana.
Watumishi wa Hazina wakishangilia baada ya mchezaji wao kuwasili kituo cha mwisho cha mbio za baiskeli cha Lake Oil mjini Morogoro jana. (Picha zote na Happiness Shayo-Utumishi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment