Waandishi wa habari waliotembelea ofisi za Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) wakipata maelezo kuhusu mafanikio ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini katika ukusanyaji wa mirabaha ya madini kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa wakala huo Bw. Bruno Mteta.
Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Usafirishaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Bw. Conrad Mtui akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya ukusanyaji wa mirabaha ya madini ya ujenzi wakati walipotembelea kituo cha ukaguzi wa madini hayo kilichopo wilayani Bagamoyo.
Mashine
ya Kuyeyusha sampuli za Madini (Fusion and cuppelation Funances), inayotumika
kwenye Maabara ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA)
(Picha zote na Fatma Salum-MAELEZO)
Na Georgina
Misama-MAELEZO
Wakala
wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa
jumla ya shilingi billioni 5.2 tangu kuanzishwa kwa wakala huo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi uzalishaji na usafirishaji wa madini Bw. Conrad Mtui wakati wa ziara ya waandishi wa habari
walipotembelea migodi ya Lugoba na Msolwa Chalinze, hivi karibuni.
“Wakala
umefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5.2 kutokana na madini hayo yaliyozalishwa
na kuuzwa na wamiliki halali wa leseni katika mikoa mbalimbali kwenye kanda za
Kaskazini, kati, Kusini, Kusini Maghalibi, Maghalibi, Mashariki na Ziwa
Victoria” alisema Mtui
Aidha,Wakala
kwa kushirikiana na Ofisi za Madini ulibuni matumizi ya “Hati ya Mauzo” kwa
lengo la kudhibiti shughuli za uzalishaji na mauzo ya madini, mkakati ambao
ulianza kutumika mwezi Juni, 2011 utakaohusisha Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Pia,
Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi
mikubwa ya madini nchini, ikiwa na lengo la kupata mrabaha na takwimu sahihi za
madini yaliyozalishwa na migodi hiyo.
Akitaja
migodi iliyofanyiwa ukaguzi alisema ni Mgodi wa dhahabu wa Geita, Golden Pride,
Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika iliyowezesha kukusanywa
kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 427.98
Akizungumzia
kuhusu hatua wanazochukuliwa baadhi ya wamiliki wa migodi wanaokiuka taratibu
za “Hati ya Mauzo” Mkaguzi wa Madini ya Ujenzi na Viwandani Abubakari Jihango
alisema kuwa hadi sasa kuna kuna kesi 53 mahakamani, na kama itadhihirika
ukiukwaji wa sheria, taratibu za kisheria zitafuatwa.
No comments:
Post a Comment