Baadhi ya watumishi wa Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao
wakati wa mashindano ya SHIMIWI dhidi ya Wizara ya Maji leo mjini Morogoro. (Picha
zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO)
Habari yazidi kuchanja
mbuga SHIMIWI.
NA Eleuteri
Mangi-MAELEZO
06/10/2014
Hoi hoi na nderemo
zimepamba moto katika viwanja mbalimbali mkoani Morogoro wakati watumishi wa
umma wakioneshana utaalamu katika michezo mbalimbali wakati wa mashindano ya SHIMIWI
inayoendelea mjini Morogoro.
Ndermo hizo zimeonekana
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo ilipofanikiwa kuingia hatua ya
robo fainali mpira wa miguu kwa kuwatoa Wizara ya maji kwa njia ya matuta
katika mchezo uliochezwa katiak nyasi za uwanja wa Mazimbu mjini Morogoro.
Mchezo huo uliisha kwa
timu hizo kufungana bao 1-1 ambapo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na
Michezo ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Wizara ya Maji dakika ya 21
kipindi cha kwanza kwa goli lililofungwa na James Mapepe wakati goli la
kusawazisha la Wizara ya Maji lilifungwa kipindi cha pili na mchezaji Alifa
Ismail katika dakika ya 40 ya mchezo.
Baada ya dakika 60 za
mwamuzi wa mchezo huo Baraka Rashidi, timu hizo zilikuwa na goli moja kila
mmoja hivyo mwamuzi huyo kwa kufuata kanuni na taratibu za mashindano hayo
aliamuru matuta yapigwe ili apatikane mshindi.
Mlinda mlango wa timu
ya likuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo Ramadhani Mtenga
ndiye aliyeibuka kuwa shujaa wa mchezo kwa kupangua penati moja na kuipa timu
yake ushindi wa penati 3 -1 dhidi ya Wizara ya Maji.
Mwamuzi wa mchezo huo
alisaidiana na washika vibendera Erick Joseph na Ramadhani Sadick wakati
kamisaa wa mchezo huo alikuwa Godifrey Evance wote wanatoka kituo cha kukuza
vipaji vya michezo cha Twalipo Youth Foundation cha mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment