Bunge nchini Rwanda limepiga kura ya kupiga marufuku BBC nchini humo, kufuatia kipindi maalum cha Televisheni kilichoitwa ''Untold story'' kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 kilichopeperushwa na BBC.
Kipindi hicho kilihoji uhusika wa baadhi ya maafisa wakuu serikalini juu ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji ya kimbari.
Bunge hilo linataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya BBC kwa kupeperusha kipindi hicho ambacho wanasema kinahujumu mauaji ya Kimbari na pia kukana mauaji dhidi ya watutsi.
Kipindi hicho kiliwahusisha wataalamu wawili wa Marekani waliohoji maelezo kuhusu mauaji ya kimbare mwaka 1994 ambayo umoja wa Mataifa unasema kuwa watu 800,000 wengi wao watutsi na wahutu wenye msimamo wa kadri waliuawa kinyama.
Hapo jana maandamano yalifanyika mjini Kigali dhidi ya BBC kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Prudent Nsengiyumva mjini Kigali.
Katika kikao kilichodumu siku nzima, wabunge pamoja na maseneta walijadili kuhusu kipindi hicho,''Rwanda’s Untold Story''
Kilipeperushwa tarehe 1 mwezi huu wa Oktoba na moja ya vituo vya BBC. Wabunge hao walitoa wito wa kusitisha matangazo ya BBC nchini Rwanda.
Wanataka serikali imchukulie hatua mtangazaji wa kipindi hicho, na wale wote waliohusika kutengeza kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment