TANGAZO


Thursday, October 23, 2014

Juhudi za kusaka chanjo ya Ebola

Chanjo ya Ebola bado haijapatikana ila juhudi zimeshika kasi kuhakikisha inapatikana
Shirika la afya duniani linatarajiwa hii leo kujadili kuhusu njia za kupata fedha za kufadhili utengezaji wa Chanjo za Ebola.
Tangu ulipotokea mlipuko wa ugonjwa huo magharibi mwa Afrika makampuni ya madawa yanaonekana kuongeza kasi ya kusaka chanjo ambayo inaweza kutumika kuzuia ugonjwa huo kuenea pamoja na tiba.
Maafisa wakuu wa makampuni hayo ya madawa , mashirika ya misaada ikiwemo MSF na shirika la afya duniani, wanakutana leo mjini Geneva kuangalia nyenzo za kufadhili utafiti wa chanjko ya Ebola.
Tayari kuna majaribio mbalimbali ya chanjo yanayofanywa katika maeneo mabli mbali ya dunia.
Zaidi ya watu elfu nne na miatano wamepoteza maisha kutokana na Ebola
Lakini watafiti wanasema huenda ikachukua miezi au hata miaka kabla ya dawa inayotibu ugonjwa huo kupatikana.
Zaidi ya watu 4,800 wamefariki kutokana na Ebola huku takriban watu elfu kumi kuambukizwa ugonjwa huo katika mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Mkuu wa tume ya muungano wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma anazuru mataifa yaliyoathiriwa na ugonjwa huo kuonyesha umoja na nchi hizo na kanda nzima ya kusini mwa jangwa la sahara.
Muungano wa Afrika unasema umeweza kupeleka mchango wake wa wahudumu wa afya katika eneo hilo ingawa bado mafanikio hayajaweza kupatikana kama ilivyotarajiwa.
Wakati huohuo, mkuu wa juhudi za dharura za umoja wa mataifa kupambana na Ebola,Anthony Banbury,alikutana na marais wa nchi tatu zilizoathirika zaidi ili kujadili mkakati wa kuhakikisha kuwa ugonjwa huo umeweza kudhibitiwa.

No comments:

Post a Comment