Kilabu
ya soka nchini Uingereza Manchester City imesema kuwa itabaini siku ya
ijumaa iwapo mechi kati yake na kilabu ya Urusi CSKA Moscow itachezwa
katika uwanja usio na mashabiki.
CSKA kwa sasa wanahudumia marufuku ya uwanja wao baada ya visa vitatu vya ubaguzi wa rangi na ghasia kuripotiwa.
Mabingwa
hao wa Urusi walicheza mechi yao ya kwanza katika uwanja wa nyumbani
katika kundi E dhidi ya Bayern Munich katika uwanja uliokuwa hauna
mashabiki.
Shirikisho
la soka barani Ulaya UEFA litakutana kuamua iwapo mechi ya Manchester
City mjini Moscow ifikiapo tarehe 21 mwezo Octoba itawaruhusu mashabiki
au la.
Mashamiki wa CSKA Moscow nchini Urusi.
Tukio
la ghasia za hivi karibuni zilizoshirikisha Mashabiki wa CSKA lilikuwa
katika ufunguzi wa mechi ya kilabu bingwa barani Ulaya mjini Roma mnamo
tarehe 17 mwezi Septemba.
Mashabiki
wa Urusi walishiriki katika ghasia hizo na polisi ambapo walirusha
cheche za moto katika uwanja wa Stadio Olimpiko baada ya kushindwa kwa
mabao 5-1.
Ghasia
hizo zinajiri baada ya matukio mawili tofauti ya ubaguzi wa rangi
katika mechi za kilabu bingwa barani ulaya ikiwemo mechi moja kati ya
CSKA na City ambapo Yaya Toure alilalamika kuhusu ubaguzi wa rangi mnamo
mwezi Octoba.
Timu
hiyo ya Urusi ilipoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Bayern siku ya
jumanne katika mechi ya iliochezwa katika uwanja mtupu.
No comments:
Post a Comment