Wanachama wa Oriflame Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja Mkazi, Fortunata Nkya wakati akielezea mambo mbalimbali ya kampuni hiyo. |
Warembo
wa Oriflame wakiwa katika sura nng'avu baada ya kutumia vipodozi
vinavyosambazwa na kampuni hiyo hakika wanapendeza, wakina mama nunueni
vipodozi vya Oriflame ili mpendeze kama akina dada hawa. Kutoka kushoto
ni mrembo Monica Mhando, Zainabu Ali na Suhaila Abdallah.
Ofisa
Mwandamizi wa Oriflame Tanzania, James Mwangamba akihojiwa na
wanahabari hapo anaelezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kampuni
hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Oriflame Tanzania inayouza vipodozi asilia
imetoa ajira kwa vijana 60,000 wa kitanzania kwa kusambaza na kuuza
bidhaa zake.
Hayo
yalibainishwa na Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya
wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla
ya kutangaza bidhaa mpya na uzinduzi wa kitabu chenye bidhaa mbalimbali
za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni
kuanzia Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.
"Tangu
tuanzishe kampuni hii mwaka 2011 tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana
60,000 jambo ambalo tunajivunia ukizingatia changamoto kubwa ya uhaba wa
ajira" alisema Nkya.
Alisema
vijana hao wamekuwa wakijipatia zaidi ya sh. milioni 10 kwa mwezi
kutokana na kufanya biashara ya bidhaa zetu kwa mfumo wa moja kwa moja.
Nkya
alisema kampuni yenye makao yake makuu nchini Sweden kila baada ya
miezi mitatu inaingiza bidhaa mpya sokoni ili kutoa fursa kwa wateja
wao kuzipata kwa urahisi na kuzisambaza kila kona kupitia mtandao wa
vijana waliopo katika makundi.
Aliongeza kuwa bidhaa nyingi ni vipodozi asilia vinavyotumika kwa wanaume na vingi zaidi ni kwa ajili ya wanawake.
Nkya
alitumia nadfasi hiyo kuwahamasisha wanawake kote nchini kununua
vipodozi kutoka Oriflame Tanzania kwani havina kemikali yoyote ni bora
na salama kwa mtumiaji kwa wakati wote.
Meneja
huyo mkazi alisema kama atahijai ufafanuzi kuhusu namna ya kuzipata
bidhaa zao anaweza kufika katika ofisi ya Oriflame iliyopo ghorofa la
Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor.
No comments:
Post a Comment