Spika wa Bunge Mhe Anne Semamba Makinda akipata maelezo toka kwa Katibu wa Bunge la Oman, Ali Nasser Al Mahrouqi ya namna mfumo wa kisasa wa uendeshaji Bunge ulivyo katika Bunge la Oman. Bunge hilo limeanza mfumo wa kutotoa hotuba/nyaraka kwa makaratasi na sasa wanatoa kwa njia ya mtandao (e-parliament).Wa pili kulia Mhe Sheikh Khalid Hilal All Maawali akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Mhe Mussa Zungu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na Spika wa Bunge la Oman Sheikh Khalid Al Maawali.Mhe William Lukuvi ambae pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni miongoni mwa wabunge nane wanaoambatana na Mheshimiwa Spika katika ziara rasmi ya kibunge nchini Oman.
Mhe. Spika Sheikh Khalid Al Maawali akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Spika Makinda kuhusu ukumbi wa Bunge la Majlis A'Shura.
Mheshimiwa Spika Anna Makinda akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Oman TV kuhusu ziara yake.
Mheshimiwa Spika akimkabidhi zawadi ya picha ya mlango wa Zanzibar Spika wa Bunge la juu la Oman Majlis Doula, Mhe. Dr Yahya Al Mandhary. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania Oman Mheshimiwa Ally Saleh.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Wabunge wenzake waliomo katika msafara. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
No comments:
Post a Comment