Meneja Uhusiano wa
Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki walipotembelea mradi wa
ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) katika
shule ya sekondari Manzese iliyopo Mtaa wa Chakula bora kata ya Manzese Wilaya
Kinondoni jijini Dar es salaam. Mradi huo unatekelezwa shuleni hapo na DAWASA
kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT).
Meneja wa Mradi wa
ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka
UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari
walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika shule ya sekondari Manzese
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi ujenzi
wa mtambo wa kuzalisha gesi ambayo ni
nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka Taasisi ya Kuendeleza
Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Shima Sago akieleza faida zitokanazo na
biogas kwa waandishi wa habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika
shule ya Sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Taaluma wa
shule ya sekondari Manzese Zubeda Kindamba akiushukuru uongozi wa DAWASA kwa
kuendelea kuiunga mkono shule yao katika masuala mbalimbali ukiwemo Mradi wa
ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi
asilia shuleni hapo.
Mwalimu wa Taaluma wa shule ya sekondari Manzese Zubeda Kindamba akiushukuru uongozi wa DAWASA kwa kuendelea kuiunga mkono shule yao katika masuala mbalimbali ukiwemo Mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi asilia shuleni hapo.
Mwanafunzi wa kidato
cha nne katika shule ya sekondari Manzese anayesoma masomo ya mchepuo wa
sayansi Noela Shirima akielezea kwa waandishi wa habari namna watakavyonufaika mara
utakapokamikika mradi wa gesi asilia itakayozalishwa na amesema kuwa kujengwa
mradi wa gesi na maabara utawasaidia shuleni hapo kwa manufaa ya kupata elimu
bora.
Meneja wa Mradi wa
ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka
UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika shule ya sekondari Manzese
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa
Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya.
Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Chakula bora Kata ya Manzes Salehe Rashidi akielezea kwa waandishi
wa habari walipotembelea shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki namna
wananchi wake wanavyoshikiana na Uongozi wa shule hiyo katika kujali taaluma ya
wanafunzi na afya zao kwa kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka shule.
Meneja Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya (wa kwanza kulia) akiwaongoza
waandishi wa habari na kujionea sehemu utakapojengwa mtambo wa kuzailsha gesi
na zinapojengwa maabara katika shule ya sekondari Manzese. Kushoto ni Meneja wa
Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas)
kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa.
Baadhi ya wanafunzi wa
shule ya sekondari Manzese wakishiriki kuandaa eneo utakapojengwa mtambo wa
kuzailsha gesi shuleni hapo.
Baadhi wa wananchi wa
mtaa wa Chakula bora wakifanya usafi kuzunguka maeneo ya shule ya Sekondari
Manzese. (Picha zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-Maelezo
SHULE ya Sekondari
Manzese inatarajiwa kunufaika na mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi
ambayo ni nishati endelevu rafiki na inayohifadhi mazingira nchini (Biogas).
Kauli hiyo imetolewa na
Meneja Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Bi. Neli Msuya juzi, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki walipotembelea
mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas)
katika shule ya sekondari Manzese iliyopo Mtaa wa Chakula bora kata ya Manzese
Wilaya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Bi. Neli alisema kuwa
mradi huo unatekelezwa shuleni hapo na DAWASA kwa kushirikiana na Shirika la
Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) ili kupata gesi ambayo pia
itasaidia upatikanaji wa umeme mbadala utakaotumika kwa matumizi mbalimbali na
kuboresha taaluma kwa wanafunzi.
Baada ya kutambua kuwa
zaidi ya asilimia 80 ya majisafi yanayotumika hugeuka kuwa maji taka, Bi. Neli
amesema kuwa endapo kiasi hicho cha majitaka kisipodhibitiwa ipasavyo neema
hiyo ya kuongezeka kwa majisafi inaweza isionekane.
“Shule haitalazimika
kufikiria majitaka hayo yaende wapi kwani DAWASA inatoa suluhisho na imechukua jukumu
la kuhakikisha maji hayo yanatumika kuzalisha gesi ambayo ni rafiki kwa
mazingira na afya za wanafunzi, walimu na wanaozunguka maeneo ya shule” alisema
Bi. Neli.
Bi. Neli ameongeza kuwa
sanjari na ujenzi wa mtambo huo wa gesi unaoendelea, pia ujenzi wa maabara kwa
masomo ya sayansi ambazo zitatumia gesi itakanayotokana na majitaka yanayozalishwa
shuleni hapo unaendelea kwa ushirikiano na UN-HABITAT ili kuboresha taaluma.
Kwa upande wake Meneja
wa Mradi huo nchini kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa amesema kuwa gesi
hiyo itatumika kwenye maabara ambazo zinajengwa shuleni hapo kuitikia wito wa
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alioutoa kuwa shule
zote ziwe zimejenga maabara kwa masomo ya Kemia, Fizikia na Biyolojia ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu.
Naye Mratibu wa Mradi
wa kujenga mtambo wa kuzalisha gesi ambayo ni nishati endelevu inayohifadhi
mazingira (Biogas) kutoka Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa
Mazingira (TaTEDO) Shima Sago amesema
kuwa kukamilika kwa mradi huo utakuwa na faida nyingi kwa shule na jamii
inayoizunguka shule hiyo.
Shima amezitaja faida
hizo kuwa ni pamoja na gesi hiyo itakuwa ya bei nafuu ambapo gharama yake ni ya
chini kutokana na malighafi kupatikana shuleni hapo na nishati hiyo
inajitosheleza kwa mazoezi ya wanafunzi maabara, kupikia kwenye kantini ya
shule, kuwasha taa kwa ajili ya wanafunzi kujisomea pamoja na ulinzi na usalama
wa shule.
Shima ametaja faida
nyingine ni kutibu majitaka yanayotokana vyoo na kuondoa athari ambazo ni
chanzo cha magonjwa hatari kwa afya za wanafunzi na jumuiya nzima inayoizunguka
shule hiyo.
Aidha, Shima amesema
kuwa gesi itakayozalishwa katika mradi huo ni ujazo wa kyubiki mita 200 ambazo
zitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kilowati 50 ambao utatosha kwa matumizi
ya shule.
Vilevile Shima amesema kuwa
mradi huo utagharamu zaidi ya Sh. Milioni
70 za Kitanzania ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka
huu tayari kuanza kutumika mwezi Januari 2015.
Kwa upande wa wanafunzi,
Noela Shirima mwanafunzi wa kidato cha nne anayesoma masomo ya mchepuo wa
sayansi amesema kuwa kujengwa mradi wa gesi na maabara utawasaidia kufanya
mazoezi mengi ameahidi kuwa watatumia muda wao vizuri ili kuboresha taaluma yao
ili waweze kufikia malengo yao waliojiwekea kwenye maisha.
Aidha, kwa kutambua umuhimu
wa uondoshaji wa majitaka, DAWASA iko mbioni kujenga mitambo yenye uwezo wa
kutibu lita milioni 241 za majitaka kwa siku katika Manispaa zote tatu za jiji
la Dar es salaam.
Mitambo hiyo itajengwa
maeneo ya Mbezi Beach (Kinondoni), Jangwani (Ilala) na Kurasini (Temeke) ambapo
wateja wakatakaounganishwa katika mfumo wa majitaka wataongezeka kutoka 18,568 hadi 25,000 mwaka 2015/2016.
No comments:
Post a Comment