Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo November, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo November (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akilipongeza Bunge la Katiba kwa kuingiza katika katiba vipengele vitatu vinavyolinda maslahi ya wanamuziki. Kulia ni Mwanamuziki, Kasim Mapili na Samatta Rajabu.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo November (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Sillian Macheche, Ofisa wa Hoteli ya Belmont, ambao wametoa ofa ya punguzo la bei kwa wanamuziki wanapohitaji kufanya jambo lolote katika hoteli hiyo, Mwanamuziki Kasimu Mapili, Samatta Rajabu na Maumbile Msanda ambao ni wanamuziki.
Mwanamuziki Kasimu Mapili (kulia), akitoa shukurani kwa Watanzania kwa msaada walioutoa kwake wakati amelazwa hospitalini wakati akitibiwa ugonjwa wa moyo. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo November.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kasimu Mapili (kulia), akiimba wakati Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo Novembar (wa tatu kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akilipongeza Bunge la Katiba kwa kuingiza katika katiba vipengele vitatu vinavyolinda maslahi ya wanamuziki. Afya ya Mapili imeimarika baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kasimu Mapili (kulia), akiimba wakati Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo Novembar (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akilipongeza Bunge la Katiba kwa kuingiza katika katiba vipengele vitatu vinavyolinda maslahi ya wanamuziki. Afya ya Mapili imeimarika baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Dotto Mwaibale
SHIRIKISHO la Muziki Tanzania (TMF), limetoa pongezi za dhati kwa Bunge la katiba kwa kuingiza vipengele muhimu kwenye Katiba mpya.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Rais wa shirikisho hilo, Addo November alisema kuwa wasanii wamekuwa wakiishi maisha magumu kabla na baada ya maisha yao ya sanaa, na kwamba kupatikana kwa katiba ya sera ya muziki itawasaidia kuwainua kiuchumi.
Aidha Addo alilipongeza bunge hilo la katiba kwa kuingiza vifungu vitatu katika katiba hiyo ambavyo ni muhimu kwenye sanaa ya muziki.
"Tunamuomba rais wetu asisite kuikubali rasimu hiyo na kuipitisha"..alisema Addo.
Pia shirikisho hilo limeingia mkataba wa makubaliano na hoteli za JB Delmont, kati ya wanamuziki na wanahabari kwa kutoa punguzo maalumu la matumizi ya huduma mbalimbali za hoteli.
Wakati huo huo,mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Kassimu Mapili ambaye ni mjumbe wa shirikisho hilo ametoa shukrani za dhati kwa ushirikiano waliouonesha wanahabari kwa na wananchi kwa ujumla katika kipindi chote alichokuwa anaumwa.
Mapili kwa muda mrefu alikuwa amelazwa akitiwa ugonjwa wa moyo ambao ulifanya asionekane katika majukwaa akifanya kazi yake ya muziki.
No comments:
Post a Comment