Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa Kampuni ya Oriflame Tanzania, Klas Kronaas, akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi fedha hizo iliyofanyika ofis za kampuni hiyo zilizopo Jengo la Benjamin Mkapa Tower Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa Kampuni ya Oriflame Tanzania, Klas Kronaas, akizungumza katika hafla hiyo.
Wanachama wa Oriflame wakimsikiliza Mkurugenzi wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa Kampuni ya Oriflame Tanzania, Klas Kronaas (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi, Mwalimu Stephania Ntaudyimara (wa pili kushoto), wa Shule ya Msingi ya Bugoyi B, kwa ajili ya kununulia madawati ya shule hiyo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya na Balozi wa Oriflame, Judith Wambura 'Ledy Jey D' ambaye ameiwezesha shule hiyo kupata fedha hizo kupitia kampuni hiyo.
Ofisa wa Oriflame Tanzania, Jesca Mwakyulu akimkabidhi zawadi ya maua Balozi wa Oriflame, Judith Wambura.
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa Kampuni ya Oriflame Tanzania, Klas Kronaas (katikati mwenye suti), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Oriflame na wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mwanachama wa Oriflame Tanzania, Christina Bazili kutoka Mabibo jijini Dar es Salaam akimpa zawadi ya maua Mwalimu Stephania Ntaudyimara.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya kusambaza na kuuza vipodozi asilia ya Oriflame Tanzania imetoa sh.milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa madawati kwa Shule ya Msingi ya Bugoyi B iliyopo mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha hizo Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki wa Kampuni ya Oriflame Tanzania, Klas Kronaas alisema msaada huo ni moja ya majukumu yao ya kusaidia jamii.
"Fedha hizi tunazo zitoa ni moja ya majukumu ya Oriflame katika kusaidia jamii tunayoihudumia katika masuala mbalimbali" alisema Kronaas.
Alisema Oriflame Tanzania imekuwa ikifanya shughuli zake karibu nchi mbalimbali za afrika na imekuwa ikisaidia kutoa ajira kwa kundi la vijana.
Alisema Tanzania hivi sasa inashika nafasi ya pili katika kutoa huduma za kampuni hiyo na tayari imetoa ajira kwa vijana 60,000.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buyogi B, Stephania Ntaudyimara alisema msaada huo umefika wakati muafaka na utasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi baada ya kupata mazingira mazuri ya kusomea.
Aliomba taasisi zingine ziige mfano wa kampuni hiyo kwa kusaidia shughuli za jamii.
Mmoja wa Wakurgenzi wa Kampuni hiyo Jesca Nisege alisema kampuni hiyo imeanzisha utaratibu wa kusomesha watoto wa wanachama wao ambao wameweza kuhamasisha watu kujiunga na Oriflame kufikia watu 21.
"Tunasomeka mtoto mmoja mmoja kwa mwanachama wetu ambaye ameweza watu wengine kujiunga na Oriflame" alisema Nisege.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment