Baadhi ya wakereketwa wa Shina la Pamba Road, wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Kivukoni, Abdalla Ally Selle 'Sosi Malema, akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere kwenye Shina la wakereketwa la Pamba Road.
Wakereketwa wa Shina la Pamba Road, wakiwa kwenye mkutano wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wakereketwa wa Shina la Pamba Road, wakiwa kwenye mkutano wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Katibu Mhamasishaji na Uenezi wa CCM Tawi la IFM, Pius Mpweza, akizunguma wakati wa maadhimisho hayo jijini leo. Wapili ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Kata ya Kivukoni, Abdalla Ally Selle 'Sosi Malema', Mwenyekiti wa shina hilo, Sharik Choughule na Katibu wake, Sophia Mbwile.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shina la wakereketwa la Pamba Road, wakifanya usafi wa mazingira, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Sharik Choughule (katikati), kwenye maeneo ya shina hilo, Posta Mpya, Dar es Salaam leo. Viongozi wa Shina hilo katika kuadhimisha Siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, wameunda kamati ya usafi itakayoshughulikia kusafisha mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Wakereketwa wa CCM wa Shina la Pamba Road, wakisafisha mazingira kwenye maeneo ya shina hilo, ikiwa ni katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wakereketwa wa Shina la Pamba Road, wakisafisha mazingira kwenye maeneo ya shina hilo, ikiwa ni katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment