TANGAZO


Tuesday, October 14, 2014

Mkutano wa Majumuisho wa Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) jijini Washington DC

Bw. Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile (hayupo katika picha), alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), jijini Washington DC, wakati wa mkutano wa majumuisho leo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni  kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania, anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu  Prof. Benno Ndulu  ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.Wakichukua mapendekezo kutoka kwa viongozi wa IMF na WB hawapo kwenye picha. Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa kamishna sera Bw. Shogholo Msangi  na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo  na  walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania.

No comments:

Post a Comment