Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha leo. (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akimpa zawadi ofisa kadeti Yusuph kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli leo.
Rais Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha leo.
Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Joseph Kabila wa DRC, wakidili jambo wakati wa hafla hiyo leo.
No comments:
Post a Comment