TANGAZO

Tuesday, October 28, 2014

Rais Kikwete Mgeni Rasmi Maadhimisho ya miaka 10 ya Utumishi wa Umma

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa kwake ambapo Kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, KatibuMkuu Kiongozi na Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea,Taasisi na Mashirika ya Umma. Kulia ni Naibu katibu wa Tume hiyo Bi NeemaTawale. (Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO)
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa  kwake ambalo litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere tarehe 30 Oktoba, 2014 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushoto ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi Rose Elipenda na kulia ni Naibu Katibu  Bi Neema Tawale akifuatiwa na Naibu Katibu Bi Rose Mboya.

Na Frank  Mvungi-Maelezo
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume  ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika jijini Dar es salam Oktoba 30 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius  K. Nyerere.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulio lenga kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo.
Akifafanua kuhusu siku hiyo Mpangala amesema Kongamano hilo la siku moja litaanza saa 2:00 asubuhi hadi 11:00 jioni ambapo pamoja na mambo mengine kongamano hilo litahusisha historia ya Utumishi wa Umma kabla na baada ya Uhuru.

“Kauli mbiu katika  maadhimisho hayo ni Imarisha Uzalendo,Uadilifu na Uwajibikaji katika Kusimamia Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma ili kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini” alisemaMpangala.

Akizungumzia wageni watakaoshiriki Mpangala amesema kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara  zinazojitegemea, Taasisi na Mashirika ya Umma, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu.
Pia Mpangala alitoa wito kwa waalikwa wote kuhudhuria  kongamano hilo kwa lengo la kuonaTume ilipotoka, ilipo na inapoelekea kwa kuyatazama mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 na mwelekeo wa Tume katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Tume ya Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) cha sharia ya Utumishi wa Umma NA. 8 ya mwaka 2002 ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 9 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa kwa sharia Na 18 ya mwaka 2007.
  
No comments:

Post a Comment