*Arejeshwa jela
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidy Benz, akiongozwa na askari Polisi kutoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, baada ya kusomewa mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidy Benz, akiongozwa na askari Polisi kutoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidy Benz, akiongozwa na askari Polisi kutoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Hata hivyo dhamani ilikuwa wazi kwa mshitakiwa huyo lakini hadi mwandishi wa bayana anaondoka mahakamani hapo ilikuwa bado kudhaminiwa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam leo, kufuatilia kesi ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidy Benz.
Askari Magereza wakimsubiri Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidy Benz na gari lao kwa ajili ya kuondoka naye Segerea baada ya kushindwa dhamana.
Grace Gurisha
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Rashid Makwaro maarufu kama 'Chidi Benz' amepandeshwa kizimbani kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi, heroin hydrochloride na vifaa vinayotumika katika uvutaji wa dawa za kulevya.
Chid Benz alifikishwa leo, mbele ya Hakimu Mkazi, Warialwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashtaka yanayomkabili ya kupatikana na dawa hizo.
Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombakono alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka matatu kukutwa na bangi, heroin hydrochloride na vifaa vinayotumika katika uvutaji wa dawa za kulevya.
Ilidaiwa Oktoba 24 mwaka huu, Chidi Benz akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam alikutwa na gramu 0.85 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride zenye thamani ya sh.38,638.
Kombakono alidai
katika shtaka la pili tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo hayo Chid benz alikutwa na gramu 1.72 za bangi zenye thamani ya sh. 1, 720.
Katika shtaka la tatu Chidi Benz anatuhumiwa kukutwa na vifaa
vinayotumika katika uvutaji wa dawa za kulevya ambavyo ni kijiko na kifuu cha nazi kinyume na sheria.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Chidi Benzi alikana kuhusika na tuhuma hizo. Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi haujakamilika.
Lema alisema ili mshtakiwa awe nje kwa dhamana anatakiwa awe na wadhamini wa kuaminika, lakini sio walimu, ambao watasaini bondi ya sh. milioni moja kwa kila mmoja.
Hata hivyo, Chid Benz alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kujikuta akipelekwa gereza la Segerea, huku wakili wake akidai kuwa zitatumika taratibu ambazo mteja wake atarudishwa tena mahakamani kwa ajili ya kudhaminiwa.
Hakimu Lema aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 11 mwaka huu kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.
Nje ya Mahakama
Ilitokea hali ya kushangaza katika eneo la Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwepo na wasanii wengi kama inavyokuwa inapotokea msanii kuwa na matatizo ya kesi.
Lakini sitofahamu ilitokea kwa mwanamuziki huyu, baada ya wasanii wenzie kuingia mitini hali iliyofanya watu waliokuwepo katika eneo hilo kujiuliza kulikoni? ambapo wengine waliishia kusema pengine walifika kukaa kwenye magari kufutilia kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment