Mkurugenzi Mkuu wa SOS Childrens Village Tanzania, Anatori
Rugaimukamu, akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya chakula cha usiku
kuchangia Watoto wa SOS na wenye mazingira magumu Tanzania, hafla hiyo
iliyoandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Montage na SOS na kufanyika
viwanja vya Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda akizungumza
katika hafla hiyo na kutoa maelezo ya malengo ya chakula hicho, cha usiku
kwa wafanyabiashara waliohudhuria hafla hiyo na kutoa malengo kiasi
cha fedha zinazohitajika kutokana na michango hiyo, kuwa kiasi cha sh. milioni 200, kusaidia watoto yatima wa SOS na wanaoishi katika mazingira magumu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya SOS Zanzibar, Bw. Mohammed Baloo,
akizungumza katika hafla hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya watoto
wa SOS na walio katika mazingira magumu.
Mtoto Tatu Haji Machano, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS Mombasa, mjini Zanzibar akitoa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata malezi katika kijiji cha sos mombasa. hadi kupata elimu ya Juu.
Mtoto Tatu Haji Machano, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS Mombasa, mjini Zanzibar akitoa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata malezi katika kijiji cha sos mombasa. hadi kupata elimu ya Juu.
Mtoto Mgeni Ali Ameir, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS mombasa
Zanzibar akitowa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili
kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata maelezo hadi kupata elimu ya
Juu katika vyuo vikuu ndani ya tanzania na nje ya nchi kwa sasa ni
Ofisa katika jumuiya ya kijamii akitumia elimu yake. aliyoipata kupitia
SOS. kwa sasa ni mama wa familia.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Bihindi
Hamad, akizungumza wakati wa hafla hiyo, ambapo pia alimkaribisha Makamu wa Rais
wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal kuzungumza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib
Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandiliwa
na Kampuni ya Montage, kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa SOS Childrens Village
Tanzania, kilichofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn, mjini Zanzibar na kuwashirikisha wafanyabiashara na Makampuni ya Umma
Tanzania.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Kijiji cha SOS Zanzibar, wakifuatilia
hafla hiyo, maalum ilioandiliwa kwa ajili ya kuchangia watoto wa SOS na
wenye mazingira magumu, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk. Bilal alipokuwa akihutubia
katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa SOS Childrens Village Tanzania wakimsikiliza Makamu wa
Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya chakula
cha usiku kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn
Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Ghari Bilal akipokea mfano wa cheki kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate Security Tanzania Bi.Jacqui Bothma, ikiwa ni mchango wao kuwachangia Watoto SOS Childrens Village Tanzania, wakatika wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto hao.kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Ghari Bilal akipokea mfano wa
cheki kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Serena Inn Zanzibar ikiwa ni
mchango wao kuwachangia Watoto SOS Childrens Village Tanzania, wakatika
wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto hao.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiungana na
Wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na
Kampuni ya Montage na SOS kwa ajili ya kuchangia Watoto wa SOS na
walioko katika mazingira magumu, hala hiyo imefanyika katika viwanja vya
hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Maofisa wa ZSSF wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku
kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchangia Kijiji cha SOS kwa Watoto walioko
katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi.Teddy Mapunda, akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Bilal, alipokuwa akiinadi picha yake, wakati wa chakula hicho.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda, akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda (katikati), akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akinadisha picha ya Makamu wa Rais Tanzania, Dk. Gharib Bilal (wapili kulia), iliochorwa na watoto wa SOS, katika wa hafla ya kuchangia iliofanyika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn Zanzibar. Picha hiyo iliuzwa kwa sh. milioni 2, katika mnada huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda, akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda (katikati), akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akinadisha picha ya Makamu wa Rais Tanzania, Dk. Gharib Bilal (wapili kulia), iliochorwa na watoto wa SOS, katika wa hafla ya kuchangia iliofanyika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn Zanzibar. Picha hiyo iliuzwa kwa sh. milioni 2, katika mnada huo.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohamed
Gharib Bilal akimkabidhi picha ya kuchora ya sura yake, iliyochorwa na Watoto wa SOS, baada ya kuinunua Mkurugenzi wa
Kampuni za Turky, Tofik Salim Turky kwa thamani ya sh. milioni 2, wakati wa hafla ya chakula cha usiku
kuchangia watoto wa Kijiji cha SOS.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Bi. Teddy Mapunda akiinadi picha ya
Rais wa Zanzibar, Dk. Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS Children Village, wakatika wa hafla
ya kuchangia iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn
mjini Zanzibar. Picha hiyo iliuzwa kwa sh. milioni moja na laki tatu.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mahomed Gharib Bilal akimkabidhi picha ya
kuchora ya Rais wa Zanzibar Dk. Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS,
Baada ya kununuliwa na PBZ kwa thamani ya shilingi milioni moja na laki
tatu kwa Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa PBZ, Seif Suleiman.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti Ofisa wa Bank Kuu ya Tanzania (BOT), Tawi la Zanzibar Ndg. Nicodemis Mboje,
kwa ajili ya kuchangia watoto wa SOS Childrens Villages Tanzania. Katika hafla hiyo zaidi ya Sh. milioni 200.9, zilipatikana.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi cheti
Meneja Masoko wa Precision Air, Azda Amani ikiwa ni shukrani kwa kuwa moja ya kampuni zilizodhamini hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Montage na SOS Children Village, Hoteli ya Serena mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi wa kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS Zanzibar wakati wa ghafla ya kuchangisha mfuko wa kuendeleza watoto yatima wa kijiji cha SOS Zanzibar iliyofanyija jana usiku Octoba 24-2014 katika ukumbi wa Serena Hotel, Jumla ya shilingi milioni 201 zilizokuwa zikihitajika zilichangishwa. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja
na wajumbe wa kamati ya uongozi wa kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS
Zanzibar pamoja na waliochangia kwa namna moja ama nyingine, wakati wa ghafla ya kuchangisha mfuko wa kuendeleza watoto yatima wa
kijiji cha SOS Zanzibar iliyofanyija
jana usiku Octoba 24-2014 katika ukumbi wa Serena Hotel, Jumla ya shilingi
milioni 201 zilizokuwa zikihitajika zilichangishwa. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanziNews) |
No comments:
Post a Comment