Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Pili Balozi wakiwa katika Mkutano wa Hadhara katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
Wananchi na Wana CCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Wananchi na Wana CCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiionesha Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa kuwaonesha wana CCM, wakati akiwahutubia wananchi na wana CCM katika Uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja katika mkutano wa Hadhara uliofanyika leo.
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika katikauwanja wa Demokrasia kibandamaiti mjini unguja wakiwa katika mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Makamo Mwenyekitiwa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali mohamed Shein
Wananchi na WanaCCM waliohudhuria katika mkutano wa hadhara Uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti wakinyoosha mikono juuu kuunga mkono maneno yaliyozungumzwa uwanjani wakati mkutano ukiendelea uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM ZanzibarDk.Ali Mohamed Shein.
Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar na mwana CCM MzeeHamid Ameir alipokuwa akitoa salama za chama kwa Wananchi na WanaCCM Kibandamaiti katika mkutano wa Hadhara uliofanyika leo na kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wananchi na WanaCCM Kibandamaiti katika mkutano wa Hadhara uliofanyika leo.
Na Said Ameir, Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar wasikubali kugawiwa
kutokana na mchakato wa Katiba unaoendelea.
Akihutubia maelfu ya wana CCM na
wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja
vya Demokrasia Kibandamaiti mjini Unguja, Dk. Shein alisema wananchi wote
waliridhia na kushiriki mchakato huo hivyo hakuna sababu ya kugawanyika baada
ya Bunge la Katiba kupendekeza Katiba Mpya.
Alisisitiza kuwa mchakato wa Katiba kamwe usiwagawe wananchi wa Zanzibar na
badala yake waendelee kudumisha amani na utulivu uliopo na kamwe wasikubaliane
na viongozi wasioitakia mema Zanzibar.
Dk. Shein aliwaeleza wananchi
hao kuwa anashangazwa na viongozi wa Chama cha Wananchi-CUF kwa kuikataa katiba
wakijua kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maslahi ya Zanzibar na watu wake.
“Napata mashaka na
viongozi wa CUF kama kweli wanataka maendeleo ya Zanzibar kwa kuwa tulipigania
wote suala la mafuta na gesi liondolewe katika mambo ya Muungano na Katiba
inayopendekezwa imefanya hivyo sasa wanachokataa ni nini?”Alihoji Dk. Shein.
Katika mnasaba huo
aliwataka wananchi kuwa makini na viongozi wa chama hicho wanapokwenda kwao kuzungumzia
suala la Katiba mpya kwa kuwa hoja zao zimekwisha ilichobaki ni kuwadanganya na
kamwe wasikubali jambo hilo.
Alisema wananchi wa Zanzibar
wana kila sababu za kuipigia kura ya ndio Katiba hiyo wakati utakapofika kwa
kuwa inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na serikali yao katika kuiletea
nchi maendeleo ikiwemo suala hilo la kuendeleza kwa sekta ya mafuta na gesi.
Dk. Shein aliwaeleza wananchi
hao kuwa Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya Zanzibar kwa ukamilifu
wake na kufafanua kuwa masuala yote yaliyokuwa yakiitwa kero za muungano yamepatiwa
ufumbuzi.
Aliwapongeza viongozi
mbalimbali waliotoa maelezo ya vifungu mbalimbali vya Katiba hiyo ambavyo
vinaonesha jinsi maslahi ya Zanzibar yalivyozingatiwa katika Katiba hiyo
ikiwemo fursa mbalimbali itakazopata Zanzibar endapo Katiba hiyo itapitishwa. Alimpongeza
pia Mzee Hamid Ameir kwa kuvunja
ukimya na kueleza juu ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964
Dk. Shein alisema kuwa mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa tanzania si jambo la kukurupuka bali ni suala la muda mrefu ambapo yeye
pamoja na Rais Jamhuri wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete walishauriana
wakati wote na kuwakumbusha wananchi kuwa suala hilo mwanzoni lilitakiwa na upinzani
wenyewe.
Katika mkutano huo Dk.
Shein aliwahakikishia tena wananchi hao kuwa Zanzibar ilishirikishwa na
kushiriki kikamilifu katika mchakato huo tangu mwanzo hadi hatua iliyopofikia
sasa kwa kuzingatia sheria ya mabadiliko ya Katiba pamoja na taratibu nyingine
zilizowekwa.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kutembelea
kifua mbele kutokana na Serikali yake kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Alirejea kauli yake
kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini mfumo wa Umoja wa Kitaifa
inatekeleza Ilani ya CCM ambayo ndio iliyoshinda uchaguzi na kuwa masuala yote
hayo ikiwemo mchakato wa Katiba umewashirikisha vingozi wote katika Serikali
hiyo.
Dk. Shein
aliwahakikishia wana CCM na wananchi wa Zanzibar kuwa chama hicho kitashida uchaguzi wa Mkuu ujao
kwa kishindo na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa chama cha CUF.
“Ushindi wa CCM
uchaguzi ujao hauepukiki na huo ndio utakuwa mwisho wa CUF na hawatakuwa na
kisingizio” alisema Dk. Shein na kuwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi ujao
utakuwa wa kidemokrasia zaidi kuliko chaguzi zilizopita.
Nae Balozi Seif Idd alimshangaa kiongozi mkubwa wa chama cha CUF kumwita
msaliti na kusema kuwa msaliti ni yeye ambaye amewatoa Wajumbe wa Katiba hiyo
ambayo ilikuwa inawatetea Wazanzibari.
Alisema kuwa Wajumbe wa CCM wa Bunge la Katiba lililopita wamemtetea Rais
wa Zanzibar ambapo kwenye Ibara ya 96 inaonesha wazi Rais wa Zanzibar kuwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nayo risala ya WanaCCM wa Mikoa
minne ya Kichama ya Unguja ilitoa shukurani kwa Wajumbe wote wa CCM katika Bunge
la Katiba na kueleza kuwa kazi kubwa na ya thamani wameifanya viongozi hao
katika kuimarisha Muungano pamoja na kuenzi Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Risala hiyo, ilieleza kuwa licha ya kuwepo kwa wapinga Mapinduzi hapa
nchini ambayo kila siku wamekuwa wakiaandaa mbinu mpya za kuyahujumu Mapianduzi
hayo kamwe hawatofanikiwa.
Aidha risala hiyo ilieleza kuwa kazi ya kuyalinda Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ni endelevu na inamuhusu kila mwana chama CCM
na kumpongeza Dk. Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete na kusisitiza kuwa
Muungano utaendelea kuwa imara.
No comments:
Post a Comment