TANGAZO


Saturday, October 25, 2014

Mke wa Waziri Membe Mama Dorca Membe atoa msaada kwa wagonjwa wa vichwa vikubwa na migongo wazi MOI


Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mama Dorcas Membe, akiongea na Seleman Joseph ambaye ni mgonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo maji  (kushoto), huku Mwenyekiti wa ASBAHT, Abdulhakim Bayakub akishuhudia.

Mkurugenzi wa Taasisi ya MOI, Dk. Othaman Kiloloma akifafanua jambo kwa Mama Membe wakati wa sherehe za watu wenye vichwa vikubwa na migongo wazi kwenye taasisi hiyo leo. Katikati ni Daktari bingwa wa magonjwa hayo, Dk. Hamisi Shabani.

Mama Membe akikata keki pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MOI, Dk. Kiloloma, Mwenyekiti ASBAHT na baadhi ya wagonjwa wa vichwa vikubwa na migongo wazi ikiwa ni katika kusherehekea siku hiyo.

Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma akimlisha keki Selemani Joseph, huku Mama Membe na Bayakub, wakipiga makofi.

Mama Membe akimlisha mtoto Amina keki wakati Mwenyekiti wa ASBAHT, Bayakub na Dk. Kiloloma wakishuhudia.

Mama Membe akimlisha mtoto anayeumwa ugonywa wa kichwa kikubwa na migongo maji keki wakati Mwenyekiti wa ASBAHT Bayakub na Dk. Kiloloma wakishuhudia.
Mama Membe akizungumza na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa vichwa vikubwa na migongo wazi (hawapo pichani).

Mama Membe akitoa msaada kwa Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma pamoja na Mwenyekiti wa ASBAHT Bayakub katika maadhimisho hayo leo.
Mama Membe akitoa msaada kwa Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma pamoja na Mwenyekiti wa ASBAHT, Bayakub.

Mama Membe akitoa msaada kwa Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma pamoja na Mwenyekiti wa ASBAHT, Bayakub. (Picha zote na Khamisi Mussa)

No comments:

Post a Comment