Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool imechabangwa nyumbani Anfield kwa mabao 3-0 kutoka kwa Real Madrid huku Mario Balotelli akiingia lawamani
Meneja wa mchezaji huyo mtukutu, Brendan Rodgers amemlaumu mshambuliaji huyo kwa kitendo chake cha kubadilishana Jezi na Pepe mara tu baada ya dakika 45 za kwanza.
Baadhi ya mashabiki wa jijini Dar es Salaam,Tanzania wamemtupia lawama mchezaji huyo ambaye pamoja na kununuliwa kwa pauni milioni 16 ameifungia Liverpool goli moja tu msimu huu.
Wakati huo huo Arsenal wamepata ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 baada ya Anderletch kuwakimbiza mchakamchaka kwa muda mrefu.
Mara baada ya mchezo huo nimezungumza na shabiki wa Arsenal ambaye anasema pamoja na ushindi walioupata lakini kuna haja ya Arsene Wenger kubadillika
Matokeo mengine ni Atletico Madrid wameifumua Malmo 5-0 na Olimpiakos imeichapa Juventus bao 1-0
Kwa upande wa michuano ya Uropa Ligi, leo Tottenham inakipiga na Asteras Tripolis, Inter Millan inakutana na St Etienne, Lille itamenyana na Evaton, wakati ambapo Viareale watacheza na FC Zurich
No comments:
Post a Comment