TANGAZO


Monday, October 13, 2014

Katibu mstaafu wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Haidary Gulamali atawazwa Ukamanda wa Vijana wa Mkoani

Aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, Haidary Gulamali akivalishwa vazi la kaniki linalotumiwa na kabila la Kigogo, wakati akisimikwa ukamanda wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoa huo, na Balozi mstaafu, Job Lusinde (kulia), huku akishuhudiwa na Kamanda wa Vijana Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru mjini humo leo. (Picha zote na John Banda)
Kamanda Gulamali akishikana mikono na vijana wa UVCCM alipokuwa akiwakabidhi Cherehani 10, viti 100 na meza 25.
Kikundi cha kwaya cha Chama Cha Mapinduzi mkoani Dodoma kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Kamanda wa UVCCM, Mkoa wa Dodoma, Haidary Gulamali  akiwa amekaa kwenye kigoda, akishikilia zana mbalimbali za kimila baada ya kusimikwa rasmi. Waliosimama ni Kingunge Ngombale Mwiru (wapili kulia) na viongozi wa Umja wa Vijana.
Balozi mstaafu, Job Lusinde (kushoto), akisalimiana na Kamanda wa Vijana Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru, mjini humo leo.
Kamanda Gulamali akishikana mikono na vijana wa UVCCM alipokuwa akikabidhi viti 100, meza 25 na cherehani 10 kwa umoja huo, ili waweze kuvitumia kama  mradi wa jumuiya hiyo, ndani ya CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Henry Msunga akizungumza jambo katika sherehe hizo. Waliokaa ni Kamanda wa UVCCM Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru (katikati) na Haidary Gulamali (kulia),  aliyesimikwa kuwa Kamanda wa Vijana Mkoa.
Baadhi ya cherehani, viti na meza zilizokabidhiwa kwa Umoja wa Vijana mkoani Dodoma na Kamanda Gulamali, mara baada ya kutawazwa kuwa kamanda wa Vijana wa chama hicho, mkoani humo leo. 
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, wakiwa katika hafla hiyo, mkoani humo leo.

No comments:

Post a Comment