.
Katika mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini
Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na
Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo
ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo
Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.
Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza
viongozi wa Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa
ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii
imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi.
Akiendelea kuzungumza Dr.
Likwelile alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na
tatizo ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti. Hili
amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo
yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano.
“ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii
inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema.
Aidha aliendela kueleza kuwa sera
ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka
baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni
changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha
kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.
Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama
yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua
kama ilivyojipangia.
Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono
miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi.
Hali ya hewa mjini hapa ni ya baridi na manyunyu
ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington
D.C
10/10/2014
No comments:
Post a Comment