Baadhi
ya wafanyakazi wa GODTEC na Bega kwa Bega Microfince wakitoa huduma katika
banda lao wakati wa Maonyesho katika
viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana
Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru
na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.
(Picha zote na Frank Shija, Tabora)
Na
Jonas Kamaleki- Tabora
Kampuni ya Godtec (T) Limted ya jijini Dar es Salaam
kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imewawezesha
vijana kufungua na kumiliki makampuni yao kwa ajili ya kujiajiri na kuajiri
vijana wengine.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa
Kanda ya Ziwa (POSO) ambayo ni moja ya
bidhaa ya Godtec, Bwana Emmanuel Kisamba wakati wa Maonyesho ya Wiki yaVijana yanayofanyika
kitaifa mkoani Tabora.
Kisamba aliongezakuwa kupitia huduma hiyo Vijana
wameunganishwa na kutengeneza Kampuni ya huduma za kifedha ya Bega kwa Bega
Microfinace Limted ambayo inamilikiwa na vijana wenyewe na kupitia Kampuni hiyo
vijana wanapata fursa kukopeshwa mitaji kwa ajili ya shughuli zaujasiriamali.
Amezitaja kampuni zilizoanzishwa chini ya utaratibu
huo kuwa ni pamoja na Consultancy in Africa (COAFRI) na Power in Africa (PAFRI),Agri-Business,
Active
Sales and Marketing zenye makao yake jijini Mwanza.
Amesema kuwa majukumu ya kamapuni hizo ni
kuwaelimisha vijana ili wajitambue na kutambua fursa zilizowazunguka
nakuzitumia ipasavyo, kuwawezesha vijana kufungua makampuni yao na kuwashauri
vijana katika miradi wanayotaka kuanzisha.
Mengine ni pamoja kuwasadia vijana
katika kuandika maadiko ya miradi endelevu nakutoa ushauri jinsi ya kufanya
biashara endelevu kwa sasa na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tunatoa mikopo kwa makampuni ya vijana na kwa
kijana mmoja mmoja”, amesema Bwana Kisamba.
Katika mikopo hiyo, dhamana ni hisa
za kampuni inayotaka kukopa. Amefafanua kuwa kila kampuni inabidi inunue hisa
kwenye Bega kwa Bega Microfinance Company Limited ambayo itafanya kampuni
lengwa kupata faida zinazotokana na Bega kwa Bega ikiwemo na kukopesheka.
Meneja huyo alisema kuwa zipo aina tatu za mikopo
ambazo alizitaja kuwa ni Anzisha, mkopo unofikia hadi shilingi milioni 5,
Imarisha, unaofikia milioni 10 na Wekeza ambao kima cha juu ni milioni 50.
Mikopo hii yote ina riba nafuu sana,wastani wa asilimia 10 kwa mwaka,
ikilinganishwa na taasisi nyingine za kifedha nchini.
Hadi sasa jumla ya makampuni manne yameshakopeshwa
na Bega kwa Bega. Meneja Emmanuel Kisamba aliyataja makampuni hayo kuwa ni
COAFRI, PAFRI, Active Sales and Marketing pamoja na Agri-business. Yote haya
yamekopeshwa jumla ya shilingi milioni 22.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa COAFRI Bw.
Ghai Edward vijana watimie fursa inayopatikana kupitia Godtec na washirika wake
kwani na kubainisha kuwa ujasiri na utayari wake baada ya kupata elimu kutoka
kwa maafisa wa Godtec ameweza kuanzisha kampuni yake na kuajiri watu wengi
hivyo amewataka vijana wasibweteke badala yake wathubutu kwa kuanzisha
makampuni.
Ghai ameongeza kuwa kwa kijana akithubutu kujiari
atakuwa amepunguza tatizo la ajira kwake mwenyewe lakini pia atakuwa amewezesha
kuongeza ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment