TANGAZO


Friday, October 17, 2014

IS:Wapiganaji wafunzwa urubani

Wapiganaji wa Islamic State
Marubani walioasi jeshi la Iraq na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State wameanza kutoa mafunzo ya urubani kwa wapiganaji IS nchini humo.
Marubani hao wanatumia ndege tatu za kivita walizoziteka kutoka kwa jeshi. Hii ni kwa mujibu wa kundi moja wa kutetea haki za binadamu la nchini Uingereza ambalo linafuatilia mgogoro huo.
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria, (SOHR) linasema mashahidi wanasema waliona ndege hizo zikiruka katika uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Aleppo.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Iraq wamefanya mashambulizi dhidi ya kambi za wapiganaji wa IS karibu na mji wa Tikrit.
Mji huo ni miongoni mwa maeneo mengine ya Syria na Iraq yaliyotekwa na kundi hilo la IS mwaka huu.
Rami Abdul Rahman,mkuu wa kundi la SOHR, amesema kuwa wapiganaji wa IS wanatumia wanajeshi wa Iraq waliokuwa wanajeshi chini ya utawala wa Saddam Hussein kutoa mafunzo kwa wapiganaji nchini Syria.
Haijulikani idadi ya wanajeshi wa jeshi la Iraq walioasi jeshi.
Waliozishuhudia ndege hizo waliambia shirika la SOHR kwamba ndege hizo zilikuwa aina ya MiG-21 au MiG-23.
Mwandishi wa BBC mjini Baghdad, Sally Nabil ameambia IS kwamba ndege tatu zilitekwa na wapiganaji wa IS kutoka kwa jeshi la Syria mjini Aleppo na Raqqa.
Mji wa Aleppo uligeuka na kuwa kitovu cha mapigano kati ya wapiganaji wa Syria ambao sasa wanajumuisha wapiganaji wa IS na wanajeshi wa serikali baada ya harakati za kumuondoa mamlakani Rais Bashar al-Assad kuanza mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment