Daktari mjini Madrid Uhispania, anasema kuwa muuguzi aliyeambukizwa Ebola amesema kuwa aligusa uso wake baada ya kumtibu kasisi aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.
Muuguzi huyo , Teresa Romero, ni mtu wa kwanza kuambukizwa ugonjwa huo nchini humo.
Makasisi walifariki kutokana na ugonjwa huo waliambikzwa wakiwa Afrika Magharibi.
Aliwauguza wanaume hoa wawili wamishionari waliofariki kutokana na Ebola nchini humo.
Awali mshauri mkuu shirika la afya duniani, alitahadharisha kwamba, wauguzi zaidi wanaowashughulikia wagonjwa wa Ebola huenda wakaambukizwa ugonjwa huo hata katika mataifa yanayostawi.
Bi Romeo, mwenye umri wa miaka 40,bado yuko Karantini nchini Hispania pamoja mumewe na watu wengine watatu.
Mtu mwingine wa tano, ambaye ni rafiki wa Romeo alilazwa hospitalini Jumatano asubuhi akiwa na joto jingi mwilini.
Inaarifiwa watu 50 wako chini ya uangalizi wa madaktari kwa hofu kuwa huenda wameambukizwa Ebola.
Muuguzi huyo, alikuwa sehemu ya kikundi cha madaktari waliowashughulikia wamishionari hao waliofariki baadaye walipohamishwa kutoka Afrika Magharibi kwenda Uhispania.
No comments:
Post a Comment