TANGAZO


Wednesday, October 8, 2014

Beckenbauer:Sikutarajia Qatar kushinda

Backenbauer
Franz Beckenbauer amebaini kwamba alishangazwa na hatua ya Qatar kushinda maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2022.
Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Ujerumani ni miongoni mwa watu 22 walioamua ni wapi kinyang'anyiro hicho cha mwaka 2018 na 2022 kitagaragazwa katika kura iliofanyika mnamo mwezi Disemba mwaka 2010.
Akizungumza katika mkutano wa kuimarisha mchezo huo mwaka 2014 ,Beckenbauer alikataa kusema ni nani aliyempigia kura ,ijapokuwa ilidaiwa kuwa alipendelea maandalizi hayo yafanyike nchini Australia.
''Ilikuwa ni kura ya siri,nilishangaa kuona Qatar ikiibuka mshindi'',Alisema mchezaji huyo mkongwe.
Mchezaji huyo wa zamani ambaye alishinda kombe la dunia kama mchezaji na meneja wa timu ya Ujerumani ,aliongezea kuwa,ushindani ulikuwa mzuri,kama ile mingine lakini hakukuwa na tofauti kubwa.
Maafisa wa shirikisho la soka la Qatar
Lazima kuna sababu kwa nini zile nchi nyengine hazikufanikiwa kuandaa mchuano huo.
Qatar iliishinda Australia,Japan ,korea kusini na Marekani katika kura ya kuandaa dimba hilo mwaka 2022,huku Urusi ikiishinda Uingereza pamoja na Unelgiji na Uholanzi,Ureno na Uhispania kwa haki ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2018.
Ni kamati kuu ya FIFA iliotoa uamuzi huo ambao umekumbwa na utata tangu tangazo hilo lifanywe.
Wanachama wawili wa zamani wa Shirikisho hilo walizuiliwa kushiriki katika kura hiyo kutokana na madai ya ufisadi,huku wengine sita wakilazimishwa kujiuzulu baada ya kura hiyo.
Backenbauer alijiondoa katika kamati hiyo mnamo mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment