Katika ligi kuu ya England jana mamilioni ya wapenda soka duniani waliokuwa wakishuhudia mtanange kati ya Chelsea na Arsenal walishuhudia Chelsea wakiibuka kidedea kwa jumla ya mabao 2-0 yakifungwa na Eden Hazard katika dakika ya 27 kwa njia ya penalti na dakika ya 78 likifungwa na Diego Costa mwenye magoli tisa katika mechi saba alizocheza katika ligi kuu hiyo ya primier.
Pamoja na mchuano uwanjani hapo lakini nao makocha wa timu hizo Jose Mourinho wa Chelsea na Arsene Wenger wa Arsenal walitifuana baada ya Wenger kulalamikia mchezo mbaya wa Cahil dhidi ya Sanchez.
Chelsea imejiimarisha kileleni kwa pointi tano juu ya Mancity inayofuatia ikiwa na pointi 14, huku Southampton akishikilia nafasi ya tatu baada ya timu zote za ligi kuu ya England kucheza mechi saba kila moja.
Kipigo cha jana cha Arsenal ni cha 12 kutoka kwa Chelsea ikiwa chini ya Mourinho dhidi ya Arsene Wenger. Mechi nyingine zilikuwa kati ya Manchester United dhidi ya Everton, ambapo Man-U imejipatia ushindi wa magoli 2-1. Tottenham imeicharaza Southampton kwa goli 1-0. Nayo Manchester City imetakata kwa kuichapa Aston Villa mabao 2-0. Msimamo wa ligi hiyo katika michezo saba, Chelsea inaongoza ikiwa na pointi 19, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 14, Southmpton ni ya tatu na pointi 13, Manchester United nafasi ya 4 sawa na Swansea zikitofautiana idadi ya magoli ya kufunga. QPR, Burnely na Newcastle ndizo tatu za mwisho zikiwa na pointi 4 kila moja.
No comments:
Post a Comment