Wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Makamu wa Rais wa Chama cha Tennis Tanzania (TTA), Fina Mango, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya vijana, umri chini ya miaka 16 na wenye ulemavu, yatakayofanyika keshokutwa, viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama cha Tennis Tanzania (TTA), Fina Mango akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya vijana, umri chini ya miaka 16 na wenye ulemavu, yatakayofanyika keshokutwa, viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo, Fouard Somi, Kulia ni Mwalimu wa timu ya Vijana, Willy Kiango na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Selcom, wadhamini wa mashindano hayo, Bupe Mwakalundwa.
Dar
es Salaam, 16 Oktoba 2014.
CHAMA cha Tennis Tanzania (TTA) kwa kushirikiana
na Gymkhana Club ya Dar es Salaam, leo wametangaza mashindano ya Tennis kwa
vijana wa umri chini ya miaka 16 na wachezaji wenye ulemavu wa miguu yaani
wheelchair.
Haya ni mashindano ya wazi
na yatatoa pointi kwa watoto watakao shiriki kwa kila kipengele
cha umri (age category) yaani chini ya umri wa miaka 16, 14 na 12. Pointi hizo
zitatokana na wingi wa ushiriki au uchache wao kama inavoainishwa kwenye
majedwali hapo chini:
Mashindano haya yamepata udhamini
kutoka kwa Selcom Wireless Limited.
Kuhusu
Selcom Wireless:
Selcom Wireless ni kampuni
ya kitanzania iliyoanzishwa Novemba 2001. Selcom imejikita zaidi kwenye
shughuli za mifumo ya elektroniki kama ulipaji wa Ankara mbalimbali kama maji,
umeme na ving’amuzi; Uwezeshaji wa matumizi ya huduma za miamala ya kibenki kwa
kupitia mitandao ya simu na benki zaidi ya 30. Selcom pia inamawakala zaidi ya 7,000
nchi nzima wanaotoa huduma za malipo mbalimbali kupitia POS na tunazidi kukua
kila siku kwa kuongeza idadi ya mawakala hawa. Na sasa Selcom inakuletea huduma
za ATM ambayo zitamuwezesha mwananchi yoyote kupitia simu yake ya mkononi na
kadi, awe na uwezo wa kufanya miamala mbali mbali. Selcom inajivunia ubunifu na
utengenezaji wa programu mbalimbali za mitandao kupitia wataalamu waliobobea na
kazi zote hufanywa ndani ya nchi. Selcom inatambuliwa na Benki kuu ya Tanzania
(BOT) kama kampuni inayoongoza nchini kwa kutoa huduma za miamala ya kibenki na
kwa mitandao ya simu kuwezesha malipo ya Ankara mbalimbali.
Kwa
kutambua umuhimu wa michezo hasa kwa vijana wadogo na watu wenye changamoto za
viungo (walemavu), Selcom imeona ni vyema kushirikiana na TTA katika mashindano
haya ili kukuza mchezo huu wa Tenis na kuupeleka hatua nyingine za kimataifa. Hii
ni mara ya kwanza kwa Selcom kushiriki na ni mategemeo yetu tatazidi kushiriki
tena na tena kwa miaka ijayo.
No comments:
Post a Comment