Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
Vijana kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakiendelea na shughuli za kufungasha mahindi na mtama kwenye magunia kwa ajili na kuyahifadhi ghalani, mazao hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.
Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.
Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma
wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama
walivyokutwa kituoni hapo jana. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
No comments:
Post a Comment