Balozi Seif akimkabidhi Mbunge wa
Singida Magharibi Mh. Alhajj Misanga Moja kati ya Seti za jezi na mipira
minne kwa timu za soka na mpira wa pete wa Skuli ya Iyumbu pamoja na
skuli ya msingi ya Ilongero. Makabidhiano hayo ameyafanya Nyumbani kwake Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma. (Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ)
Na Othman Khamis Ame, OMPR
MAKAMU wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Wabunge na Viongozi wa
Mkoa wa Singida kwa kazi kubwa wanazoendelea kuzifanya za kusimamia
miradi ya Kiuchumi na ustawi wa Jamii ya wananchi wa Mkoa huo.
Amesema usimamizi huo
umeufanya Mkoa huo kuongezeka harakati za maendeleo jambo ambalo
wananchi walio wengi wameonyesha muelekeo mkubwa wa kujitegemea
kimaisha.
Balozi Seif alisema
hayo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi michango na kupunuza ahadi
alizozitoa wakati wa ziara yake ya hivi karibuni Mkoani Singida
aliyoifanya rasmi kuaga kama Mlezi wa Mkoa huo Kichama.
Akikabidhi michango
hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. John Chiligati na
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe. Alhajj Misanga hapo nyumani
kwake Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma Balozi Seif alielezea masikitiko
yake kwa kuukosa ukarimu wa Wananchi wa Mkoa huo aliouzoea wakati wa
ulezi wake.
Balozi
Seif aliwakumbusha Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Singida kuendelea
kushikamana na yeye atakuwa tayari kuongeza msukumo wake ili kuona
maendeleo ya Kijamii yanazidi kukua na kustawisha ustawi wa jamii ya
wananchi wa Mkoa huo.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Singida Mbunge wa Jimbo la
Singida Mashariki Mh. John Chiligati alisema Balozi Seif Ali Iddi
alifanya kazi kubwa iliyoleta mshikamanio wakati akiwa Mlezi wa Mkoa huo
wa Singida.
Mh.
Chiligati alisema Balozi Seif amekiacha Chama cha Mapinduzi imara ndani
ya Mkoa wa Singida na wakaahidi kwamba malezi mema aliyoyaacha
watajitahidi kuyaendeleza ipasavyo.
“Ukweli tumesikitika kumkosa mlezi muadilifu aliyetuachia majonzi
kutokana na uitendaji wake. Lakini hata hivyo tumemuwekea milango wazi
awe huru kushauri na kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi wa
Singida “. Alisema Mh. John Chiligati.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Singida Masharik pia limpongeza na kumshukuru Mke wa
Mlezi huyo Mstaafu wa Mkoa wa Singida Mama Asha Suleiman Iddi kwa
msimamo wake wa kusimamia ilani na sera za Chama cha Mapinduzi
Kivitendo.
Mh. Chiligati alimuelezea Mama Asha kuwa ni jasiri
kutokana nay eye pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein kuuongoza Umoja wa wake wa Wabunge na Wawakilishi wa CCM Zanzibar
ambao umeleta mafanikio makubwa hasa kwa akina mama na watoto.
Balozi
Seif katika hafla hiyo fupi alikabidhi mchango wa shilingi Milioni moja
na laki Tano kwa ajili ya ununuzi wa mabati ya kuezekea jengo la Mabara
ya Skuli ya Sekondari ya Chikuyu iliyopo Wilaya ya Manyoni,shilingi
1,000,000/- za kununulia matofali kwa uendelezaji wa Kituo cha Afya cha
Kijiji cha Mtunduru pamoja na shilingi 1,000,000/- kwa ajili ya Madrasa
ya Muzdalifa iliyopo Ilongero.
Balozi
Seif pia akakabidhi zawadi za Seti moja moja za Jezi na mipira minne
kwa timu za soka na mpira wa pete wa Skuli ya Iyumbu pamoja na skuli ya
msingi ya Ilongero.
No comments:
Post a Comment