Ofisa Tawala wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) Bw. Peter Ugata akitoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla kutumia wakala huu unaowaunganisha waajiri na watafuta kazi nchini.wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wakala huo Bi. Jamila Mbaruku. (Picha zote Hassan Silayo-MAELEZO)
Frank
Mvungi- Maelezo
WAKALA
wa huduma za ajira Tanzania (TaESA) watoa mafunzo kwa watafuta kazi 2146 katika harakati za kuwaunganisha watafuta
kazi na waajiri hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wakala huo Bi Jamilah
Mbarouk wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua
Bi Jamilah amesema kati watafuta kazi waliopatiwa mafunzo hayo wanaume ni 1254
na wanawake ni 879.
“Vile
vile wakala umeweza kutoa mafunzo haya kwa vyuo vitano (5) ambavyo ni Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE)Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu
(TIA),Chuo cha ardhi na Taasisi ya ya Teknolojia Dar es salam ambapo vyuo vyote
viko Dar es salaam na kushirikisha wanavyuo 860.”alisema Jamilah.
Kwa
sasa mafunzo haya hutolewa kila ijumaa kwa watafuta kazi waliosajiliwa TaESA.
Katika
kutoa mafunzo hayo TaESA imelenga
kuwajengea uwezo watafuta kazi kuwajengea uwezo na ujuzi wa kuandika barua za
maombi ya kazi,jinsi ya kufanya usaili
kwa kujiamini na kuelewa kuhusu matarajio ya waajiri kwa wafanyakazi.
Wakala
wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsa) ulianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 30 ya
mwaka 1997 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2009) na kuzinduliwa rasmi tarehe 16
june,2008 kufuatia tamko la Serikali Na.189 la mwaka 2008 na kuanza shughuli
zake tarehe I julai,2008 ikichukua nafasi ya kilichokuwa kituo cha ajira nchini
(Labour Exchange Centre).
No comments:
Post a Comment