*Arejea Nyamisati kwa boti ya kizamani

Katibu Mkuu wa CCM akipanda boti hiyo kwa ukakamavu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye boti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, ambaye aliwasili wilayani Mafia kwa ndege lakini akalazimika kusafiri na Kinana kwa boti hiyo kurejea Nyamisati. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao.
Katibu wa NEC, Itikadina Uenezi, Nape Nnauye (watatu kushoto), akiwa kwenye boti na abiria wengine waliosafiri pamoja na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
Baadhi ya maofisa wa CCM na Waandishi wa habari wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo (watatu kushoto) akiwa na abiria wenzake katika boti hiyo kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
Abiria wengine wakiwa katika boti hiyo kutoka Mafia kwenda Nyamisati leo. Kushoto ni Mwandishi wa Clouds TV/Radio Salum Mwinyimkuu.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mama Salma Kikwete ya Wama iliyopo wilayani Rufiji, baada ya kutoka Mafia. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Suma Mesa. Kinana amempongeza Mama Salma kwa uamuzi wake wa kuanzisha shule hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto yatima kutokamikoa mbalimbali nchini.
Watoto wa shule hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kinana.

No comments:
Post a Comment