Waziri wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Mhe.
Mhandisi Dkt.
Binilith Mahenge akiongea na waandishi wa habari, mjini Dodoma, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka
la O zoni litakalofanyika Septemba 16, 2014 nchini.
(Picha zote na Benedict Liwenga,
MAELEZO-Dodoma)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifauatilia kwa makini
maelezo toka kwa Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge yaliyohusu Maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni litakalofanyika Septemba 16, 2014 nchini.
Waandishi wa habari wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge, kuhusu Maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yatakayofanyika Septemba 16, 2014 nchini.
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma
TAREHE
16 Septemba, mwaka huu Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa
katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama
ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la
49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe.
Mwandisi Dkt. Binilith Mahenge wakati alipofanya mkutano na waandishi wa
habari 15 Septemba, 2014 kwa lengo la kuongelea juu ya Maadhimisho hayo
linalofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Mwandisi Mahenge ameeleza kuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
Ameendelea
kwa kusema kuwa Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza
zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji
na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
“Punguzo
hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni
pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani”, alisema Dkt. Mahenge.
Akizungumzia
kuhusu mikakati ya kitaifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa
Mkataba huo, Dkt. Mahenge alisema kuwa 1996 Serikali iliandaa na
kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali
zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, mikakati hiyo ni pamoja kujenga uwezo
wa Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa Mkataba, kuweka
takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu
umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari
kuhusu kemikali na teknolojia mbadala na mikakati mingineyo.
“Hatua
hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba
iliyowekwa na Mkataba”, alisema Mhe. Mwandisi Mahenge.
Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi
yaani (Refrigerant Management Plan) na
katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa
Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni
ambazo zilianza kutumika tarehe 7 Desemba mwaka 2007, kusambaza kwa
Vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo
mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia
majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi
chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu
na viyoyozi hapa nchini.
Aliongeza kuwa hadi sasa, Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86% ya kiasi cha matumizi ya kemikali
hizo, mwaka 1999.
Hapa
nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu
Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hilo na
matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa tabaka la ozone.
No comments:
Post a Comment