TANGAZO


Monday, September 15, 2014

Adha ya mvua maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam


JIJI la Dar es Salaam leo, limegeuka kuwa adha baada ya mvua kunyesha na kusababisha kutuama kwa maji katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Hali hiyo, ilisababisha wananchi na wageni mbalimbali waliokuwa wakipita maeneo ya Posta Mpya kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufika kule waendako.

Kwa wale waliokuwa wakifanya shughuli zao maeneo hayo, walilazimika kuaghirisha shughuli zao hizo hadi majira ya saa 9 Alasiri, mvua ilipopungua pia maji yaliyokuwa yamesambaa kuondoka kwa baadhi ya maeneo hayo na kubakisha yaliyokuwa yametuama kwenye madimbwi kwenye Barabara la maeneo hayo.
Picha za china zinathibitisha hali hiyo katika maeneo hayo kama zilivyoandaliwa Dotto Mwaibale wa mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wananchi wakipita kwenye dimbwi la maji maeneo ya Posta Mpya
Kijana akipita kwenye dimbwi hilo huku akisukuma tolori lake lenye madumu.
Maji yakiwa yameeneo katikaeneo hilo karibu na kituo cha kuuzia mafuta.
Kijana akipita kwenye dimbwi hilo mbele ya maegesho ya Tax katika eneo hilo.
Mwendesha baiskeli ya magurudumu matatu akipita eneo hilo.

No comments:

Post a Comment