Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo (kushoto), akiwa na Fahmy Dovutwa.
Na Magreth Kinabo, Dodoma
11/09/2014
MJUMBE wa
Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti
wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD)Mhe. John Cheyo amesema kwamba mchakato
mzima wa Katiba utamalizwa kwa kura ya maoni ya wananchi, hivyo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya
Kikwete haiwezi kutamka leo kulihairisha Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa
liko Kisheria.
Aidha Mhe.
Cheyo alisema kilichoahirishwa ni mchakato wa kura ya maoni ya wananchi na si
Bunge hilo kwa kuwa walikubaliana katika kikao cha mashauriano, baina Rais Kikwete
na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge
vinavyounda TCD kuwa bunge hilo liendelee.
Kauli hiyo
imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Mhe. Cheyo wakati wa mjadala wa kujadili
sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo alisema hayo ndiyo
makubaliano yaliyofikiwa.
Aidha Mhe. Cheyo alisisitiza Katiba Mpya
inayopendekezwa itakayopatikana itadumu kwa njia ya maridhiano.
“ Bunge hili
linaendeshwa kwa mujibu wa sheria , Tangazo la
Serikali (Government Notice) Na 254 hili ndilo uhai wa Bunge hili hadi
Oktoba 4, mwaka 2014, na wote tukakubaliana haiwezekani Mhe.
Rais akasema leo Bunge likasitishwa.
“ Vitu
viwili vikukutana kwa nia ya maridhiano,
vitu vingine vinaweza kuwekwa pembeni sawa na sasa na baadae vinaweza
vinashughulikiwa kwa wakati huo,” alisema Mhe. Cheyo.
Mhe. Cheyo
alisema anamwomba Rais Kikwete atoe
ruhusa ya kuwepo kwa kipindi maalum cha
kitakachorushwa na televisheni (video) ili kila mtu aonekana alichokisema, huku akionesha kusikitishwa na
upotoshwaji wa makubaliano hayo, uliofanywa na baadhi ya wanasiasa.
“ Mojawapo
ambayo tuliyokubaliana Bunge hili
lipate Katiba ambayo inapendekezwa na wananchi pia kwa hali tulinayo
haiwezekani mchakato mzima ukamalizika,
mchakato utamalizika kwa kura ya maoni ya wananchi. Kama tukifika huko itabidi
tuhairishe uchaguzi wa mwaka 2015. Niliyoyasema
ndiyo makubaliano tuliyokubaliana,” alisisitiza.
Mhe. Cheyo
alisema Rais Kikwete alikubali kukaa chini pamoja na TCD na hao wanaojiita
Ukawa.
Alisema
Rais Kikwete alifanya mazungumzo na
viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD mara
kwa mara ya kwanza, Agosti 31, mwaka 2014 kwa saa nne na mara ya pili,
Septemba 8, mwaka 2014 kwa saa mbili.
Kikao hicho
cha mashauriano kilihusisha kamati ya makatibu
wakuu, kamati ya wenyeviti wa vyama vya CCM, CHADEMA,CUF na NCCR- Mageuzi.
No comments:
Post a Comment